Saturday, October 19, 2013

MFANYABIASHARA MWENYE ASILI YA ASIA AKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI

Ben Komba/Pwani-Tanzania

Kibaha tarehe 18 Octoba, 2013. Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia
Shehe Mohamed Saqib umri miaka 37,kabila Punjab raia wa Asia
mfanyabiashara, mkazi wa Block 41 Oyesterbay Namanga Dar es Salaam kwa
kosa la kukutwa na nyara za serikali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina Msaidizi Ulrich Matei
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameeleza kuwa Shehe Mohamed
alikamatwa kwenye kizuizi kilichowekwa na askari wa kikosi kazi maalum
eneo la Mwandege Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, wakiwa kwenye
Oparesheni Okoa maliasili inayoendelea Mkoa wa Pwani.
Kamanda Matei ameeleza kuwa Shehe Mohamed Saqib, baada ya kukamatwa majira
ya saa 08:00 usiku na askari hao waliopo katika Oparesheni hiyo kutoka
Mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam pamoja na Zanzibar alikutwa akiwa na
Risasi 32 za silaha aina ya Rifle 270 na kipande cha nyama aina ya Swala
kwenye gari No. T448 AVM aina ya Toyota Land Criser, akisafirisha toka
Wilaya ya Rufiji kwenda Dar es Salaam.
Baada ya Askari hao kumkamata walikwenda kumpekua nyumbani kwake nakumkuta
akiwa na mikia ya Tembo vipande nane (8), kucha za Simba 19, Sare za Jeshi
la wananchi wa Tanzania Jozi 5 na suruali 2, Sare za Tanapa suruali 3 na
koti 1, Sare za wanyama pori suruali 1 na kikoti, Silaha aina ya Rifle 240
na Risasi zake 21, Silaha aina ya Rifle 270, Silaha aina Shot gun Pump
Action na Risasi 10, Risasi 2 za Silaha aina ya Shot Gun two pipes,
vipande 3 vya nyama ya Nyumbu, fuvu la kichwa cha Nyati, kichwa cha Swala
Pala, na kipande cha nyama ya Kongoni.

No comments:

Post a Comment