Tuesday, April 15, 2014

HATUA NZURI KUELEKEA KWENYE SIKUKUU YA PILI KATIKA MAISHA YA MWANADAMU

 Ilikua ni siku muhimu kwa Mdau MKUBWA wa blog hii www.habarizamitaa.blogspot.com alipoamua ku-"propose"

Ilianza kama hivi

 
"Baby tupozi kidogo wenye wivu wajinyonge"


 
Sasa baby mimi nataka niifanye iwe "official" au unasemaje baby


 

Unaona nipo "serious"

 

Ndio hii honey wangu

 

Ishara hii ndo iwe kithibibisho kwamba nia yangu ni kufanya "kweli"

 

NIKUBUSU KWA UPENDO

 
TAYARI YAMEKUA 


MAKOFI TAFADHALI...........PWAAA.....PWAAAAA...... PWAAAAA

Monday, April 14, 2014

MAFURIKO YALIVYOTESA RUVU DARAJANI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-4-2014
Mvua kubwa zilizonysha kwa siku tatu mfululizo zimeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika mkoa wa Pwani, ambapo barabara kuu ya Morogoro madaraja mbalimbali yametitia kutokana na mvua hiyo kubwa ambayo imesababisha madhara makubwa kwa miundombinu.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia msongamano mkubwa wa malori na magari ya abiria yakiwa yamejipanga kufuatia kukatika kwa kipande cha barabara eneo la Ruvu na kusababisha magari kushindwa kupita eneo hilo na kuzxua foleni kubwa ambayo imeanza kupitisha magari madogo.
Nayo serikali haikuwa nyuma kupitia kikosi cha ujenzi barabarani imefanya kazi kubwa kukarabati maeneo ambayo yamekumbwa na uharibifu uliosababishwa na mafuriko makubwa ya maji ambayo yalifunika kabisa barabara ya Morogoro na kufanya shughuli za usafirishaji na uchukuzi kusimama kwa takriban masaa 72.
Uharibifu huo haukubaki barabara kubwa ya Morogoro, bali hata shamba la ushirika la kilimo cha umwagiliaji Ruvu wilayani Bagamoyo-CHAURU- nalo limeathirika kwa kiasi kikubwa na mvua hizo, kwa madaraja mawili kukatika na kuwafanya wakulima kuamua kutumia jitihada zao kukarabati maeneo korofi huku wakiitaka serikali kutupia macho madhara yaliyosababishwa na mvua hizo.
Makamu mwenyekiti wa ushirika huo wa kilimo mpunga kwa njia ya umwagiliaji-CHAURU- BW.MSIRIKAL;I amebainisha kuwa mpaka sasa wameomba makaravati kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani ili waweze kukarabati maeneo korofi na kuepukana na adha zilizoletwa na mvua hiyo.

Akizungumzia uharibifu wa mazao hususan ya mpunga, BW.MSERIKALI amebainisha kuna uwezekano mkubwa wa kupungua kwa mavuno iwapo mvua hizi zitaendelea, kwani mpaka sasa kuna uharibifu mkubwa wa matuta ya mifereji ambayo inatumika katika shamba hilo.
Ameiomba serikali kupitia wataalamu wake kuungana na wanachama wake kusaidiana kurudisha hali ya barabara hiyo inayotumika kuingia na kutoka shamba hilo ambalo ni maarufu kwa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji.


MVUA

Sunday, April 13, 2014

BOMU MIANZINI

Umesikika mliouka wa Bomu maeneo ya baa maarufu ya MATAKO BAR na watu zaidi ya 15 wamejeruhiwa. Tutawajulisha kadiri tutakapo pata habari zaidi

Friday, April 11, 2014

TUKIO MAENEO YA MOROCO JUNCTION

Umetokea uhalifu mchana wa Leo baada wapanda pikipiki kumshambulia RAIA kwa risasi na kisha kupora kiasi cha fedha ambacho thamani yake haijajulikana.

TRENI YA UBUNGO YAACHA RELI......

Treni ya Ubungo maarufu kama treni ya Mwakyembe. Imepata ajali jioni ya Leo ilipokua ikiwasili kituo cha "daresalaam station" baada kuacha reli yake " line one" na kuzivuka reli zingine mbili.

Monday, March 31, 2014

UFAFANUZI WA BAKWATA

Mufti wa Tanzania,Sheikh Issa Shaaban bin Simba,hakusema alivyoripotiwa. Hakusema kuwa BAKWATA inapinga uwepo wa Serikali tatu. Nikiwa namwona,kumsikia,kumsikiliza na kumwelewa,Mufti Simba alikaripia jambo moja kubwa. Ingawa hakumtaja,alidai kuwa kuna mtu anasema Waislam wanataka Serikali tatu.Alichosema Mufti Simba ni kuwa huo si msimamo wa Waislam wote. Ndiyo maana alijitokeza kuweka mambo sawa.

Alichosisitiza Mufti Simba ni kuwa Waislam na umma wa Tanzania wanataka aina moja tu ya Katiba:ile ambayo itadumisha amani,utulivu na mshikamano baina ya watanzania. Katiba bora kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo. Hakuna mahali ambapo Mufti Simba alitaja kukubali au kukataa aina ya Muungano. Hakuna mahali aliposema hataki au BAKWATA hawataki Serikali tatu.

Ifike wakati,tuwanukuu viongozi wetu (hasa wa kidini) kama walivyosema. Hawa ni watu tegemezi kwetu na wanamadhara makubwa kama wakinukuliwa vibaya. Ikiwezekana iwekwe santuri ya sauti yao ili ukweli ujulikane.Upotofu katika wakati kama huu ni wa kuogopwa kama ukoma.