Monday, April 14, 2014

MAFURIKO YALIVYOTESA RUVU DARAJANI

Ben Komba/Pwani-Tanzania/14-4-2014
Mvua kubwa zilizonysha kwa siku tatu mfululizo zimeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli mbalimbali za uzalishaji mali katika mkoa wa Pwani, ambapo barabara kuu ya Morogoro madaraja mbalimbali yametitia kutokana na mvua hiyo kubwa ambayo imesababisha madhara makubwa kwa miundombinu.

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia msongamano mkubwa wa malori na magari ya abiria yakiwa yamejipanga kufuatia kukatika kwa kipande cha barabara eneo la Ruvu na kusababisha magari kushindwa kupita eneo hilo na kuzxua foleni kubwa ambayo imeanza kupitisha magari madogo.
Nayo serikali haikuwa nyuma kupitia kikosi cha ujenzi barabarani imefanya kazi kubwa kukarabati maeneo ambayo yamekumbwa na uharibifu uliosababishwa na mafuriko makubwa ya maji ambayo yalifunika kabisa barabara ya Morogoro na kufanya shughuli za usafirishaji na uchukuzi kusimama kwa takriban masaa 72.
Uharibifu huo haukubaki barabara kubwa ya Morogoro, bali hata shamba la ushirika la kilimo cha umwagiliaji Ruvu wilayani Bagamoyo-CHAURU- nalo limeathirika kwa kiasi kikubwa na mvua hizo, kwa madaraja mawili kukatika na kuwafanya wakulima kuamua kutumia jitihada zao kukarabati maeneo korofi huku wakiitaka serikali kutupia macho madhara yaliyosababishwa na mvua hizo.
Makamu mwenyekiti wa ushirika huo wa kilimo mpunga kwa njia ya umwagiliaji-CHAURU- BW.MSIRIKAL;I amebainisha kuwa mpaka sasa wameomba makaravati kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani ili waweze kukarabati maeneo korofi na kuepukana na adha zilizoletwa na mvua hiyo.

Akizungumzia uharibifu wa mazao hususan ya mpunga, BW.MSERIKALI amebainisha kuna uwezekano mkubwa wa kupungua kwa mavuno iwapo mvua hizi zitaendelea, kwani mpaka sasa kuna uharibifu mkubwa wa matuta ya mifereji ambayo inatumika katika shamba hilo.
Ameiomba serikali kupitia wataalamu wake kuungana na wanachama wake kusaidiana kurudisha hali ya barabara hiyo inayotumika kuingia na kutoka shamba hilo ambalo ni maarufu kwa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji.


No comments:

Post a Comment