Monday, March 31, 2014

UFAFANUZI WA BAKWATA

Mufti wa Tanzania,Sheikh Issa Shaaban bin Simba,hakusema alivyoripotiwa. Hakusema kuwa BAKWATA inapinga uwepo wa Serikali tatu. Nikiwa namwona,kumsikia,kumsikiliza na kumwelewa,Mufti Simba alikaripia jambo moja kubwa. Ingawa hakumtaja,alidai kuwa kuna mtu anasema Waislam wanataka Serikali tatu.Alichosema Mufti Simba ni kuwa huo si msimamo wa Waislam wote. Ndiyo maana alijitokeza kuweka mambo sawa.

Alichosisitiza Mufti Simba ni kuwa Waislam na umma wa Tanzania wanataka aina moja tu ya Katiba:ile ambayo itadumisha amani,utulivu na mshikamano baina ya watanzania. Katiba bora kwa mustakabali wa maisha yetu na vizazi vijavyo. Hakuna mahali ambapo Mufti Simba alitaja kukubali au kukataa aina ya Muungano. Hakuna mahali aliposema hataki au BAKWATA hawataki Serikali tatu.

Ifike wakati,tuwanukuu viongozi wetu (hasa wa kidini) kama walivyosema. Hawa ni watu tegemezi kwetu na wanamadhara makubwa kama wakinukuliwa vibaya. Ikiwezekana iwekwe santuri ya sauti yao ili ukweli ujulikane.Upotofu katika wakati kama huu ni wa kuogopwa kama ukoma.

No comments:

Post a Comment