Saturday, October 19, 2013

AJALI

Ben Komba/14-10-2013/11:51

(i) Ajali ya kusababisha vifo / majeruhi:- Tarehe 13/10/2013, majira ya
saa 2.45 asubuhi huko maeneo ya Kwa Kipofu Visiga barabara ya kuu ya Dar
es Salaam – Morogo (W) Kibaha (M) Pwani. Gari Na. T.324 AWR aina
Mitsubishi Canter likiendeshwa na John Joseph Mkombozi umri miaka 50,
mkazi wa Ifakara Morogoro akitokea Dar es Salaam kwenda Ifakara aligongana
uso kwa uso na gari Na. T.180 AWT aina ya Toyota Caldina saloon iliyokuwa
ikiendeshwa na dereva mwanamke aitwaye Mwaitulo Suma Andelwisye, umri
miaka 36 mfanyakazi wa SUA Morogoro na kusababisha vifo kwa watu watano
akiwemo dereva huyo na abiria wengine wanne ambao majina yao bao
kufahamika, jinsia zao ni wanaume wawili moja anakadiriwa kuwa na umri wa
miaka 10, mwingine umri miaka 2½, wakike watatu moja ni dereva wa gari
hilo, mwingine anakadiriwa kuwa umri wa miaka 18, mwingine umri wa miaka
minne. Marehemu wote walikuwa ndani ya gari Na. T.180 AWT aina ya Toyota
Caldina saloon. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha
ikisubiri kufanyiwa uchunguzi na Daktari kutambuliwa na ndugu. Pia katika
ajali hiyo majeruhi ni wawili ambao walikuwa kwenye Gari Na. T.324 AWR
aina Mitsubishi Canter ambao ni Hilda d/o Magoda umri miaka 29, mhehe,
mfanyabiashara, na Farida d/o Hassan umri miaka 31, mfanyabiashara wote
mkazi wa Mbezi kwa Msuguri Dar es Salaam, wamelazwa Hospitali ya Tumbi
Kibaha wakiendelea na matibabu zaidi. Chanzo cha ajali ni marehemu
kuovateki sehemu isiyoruhusiwa bila uangalifu.Majina ya marehemu wengine
yatafuata baada ya kutambuliwa na ndugu.

(ii) Kujinyonga:- Tarehe12/10/2013, saa 12:00 jioni, huko Kijiji cha
Mandela Kibaoni Kata ya Mandela Tarafa ya Miono (W) Bagamoyo (M) Pwani.
Francis Ngoli umri miaka 85, mkulima mkazi wa Kijiji cha Mandela alikutwa
amejinyonga kwa kutumia kamba ndani ya nyumba yake aliyokuwa akiishi peke
yake baada ya kufiwa na mke wake miaka miwili iliyopita. Chanzo cha
kujinyonga bado kujulikana / kinachunguzwa. Mwili wa marehemu umefanyiwa
uchunguzi na Daktari na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.

(iii) Kifo cha mashaka:-Tarehe 13/10/2013, majira ya saa 12.300 asubuhi
huko Kwa Zoka kandokando mwa barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro (W)
Bagamoyo, (M) Pwani. Umekutwa mwili wa marehemu asiyefahamika mwanaume
umri kati ya miaka 20 – 25 ukiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha
kali kwenye paji la uso wake. Inasadikiwa marehemu ni moja kati ya vijana
wenye tabia ya kupora mizigo kwenye malori ya mizigo. Mwili wa marehemu
umehifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha ukisubiri kufanyiwa uchunguzi na
Daktari / kutambuliwa na ndugu.

No comments:

Post a Comment