Friday, August 16, 2013

KWANINI MWANAMKE?
Katika mikutano mbalimbali ya kiroho ambayo kwa rehema za MUNGU nilifanikiwa kuhudhuria nimekua nikiona wara ifikapo saa ya MAOMBEZI idadi ya wanaoanguka kati ya WANAUME na WANAWAKE, idadi kubwa ya watakao anguka ni WANAWAKE.
SWALI KWANINI WANAWAKE?
1.-KUIANGUSHA JAMII
Kwanza tuanze kutazama historia kuanzia kwa “MAMA YETU EVA/HAWA” tukisoma kitabu cha MWANZO 3 tutaona namna ambavyo shetani na mwanamke wakiwa katika mazungumzo ambayo mwisho wa “mazungumzo” yale nyoka anafanikiwa kumhadaa na mwanamke anakula TUNDA NA ANAMWEKEA NA MUMEWAKE ambapo baadae tunakuja kuambiwa ndio mwanzo wa ANGUKO LA MWANADAMU.
--huu ni ushahidiwa namna ambavyo ADUI ANAWEZA KUMTUMIA MWANAMKE KUISHAMBULIA JAMII

2.KUIINUA JAMII
Ukikisoma vizuri kitabu cha ESTA (ambaye ni mwanamke) utaona namna ambavyo MUNGU alivyo mtumia mwanamke KUWAOKOA WATU WAKE NA UDHALIMU WA HAMANI na mwisho hamani akafa na WATU WA MUNGU WAKAPATA UKOMBOZI.
KWANINI MWANAMKE?
Ukisoma kitabu cha UFUNUO 12 utaona shetani /joka akijaribu kupambana na MWANAMKE na UZAO WAKE. UFUNUO 12: 17  Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.
Ukisoma UFUNUO 12 yote utaona hadithi kamili ya namna ilivyo kuwa
JIBU: MWANAMKE ni mshirika wa KARIBU NA WA MUHIMU SANA katika ulimwengu kwasababu ndipo uzao/ uzazi hutunzwa kwa MWANAMKE kwa njia ya mimba. Na kitaalam MIMBA ilioko tumboni mwa MWANAMKE huwa na muunganiko wa mojakwa moja kwa njia ya DAMU muunganiko ambao hauepukiki. Hivyo basi kupitia kwa mwanamke VIBAYA NA VYEMA HUPITA HAPO.
Hivyo shetani anawashambulia sana WANAWAKE KWA MAANA AKIFANIKIWA KUWAPATA NA KUWAHARIBU (DESTRUCT) WANAWAKE tayari atakua ameuharibu ULIMWENGU.

THEME:
WANUME TUWALINDE WANAWAKE kwa MAOMBI na malezi mema ili shetani asipate nafasi katika maisha yao ILI ISIWE CHANZO CHA UHARIBIFU.

WANAWAKE
WEWE NI CHOMBO MUHIMU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NA MWILI HIVYO
Mjilinde na kila lisiliojema  MAANA MNADHAMANA YA KUUZAA ULIMWENGU NA KUUFANYA SEHEMU SALAMA
MUNGU AWABARIKI, AWALINDE NA KUWAONGOZA WANAWAKE ILI SHETANI ASIPATE NAFASI KATIKA ULIMWENGU NA FAMILIA ZETU NA JAMII ZETU.


MARKO MANGARA MATHIAS

No comments:

Post a Comment