Saturday, August 17, 2013

UNANINI EWE ULALAYE USINGIZI?

UNANINI EWE ULALAYE USINGIZI?

Nchi yetu inapita katika vipindi mbalimbali vigumu na ambavyo hatukuwahi kuvipitia kabla. Chuki imeongezeka kwa kiwango cha ajabu na watu huchekeana tu kwasababu ya MAZOEA TU. upendo wa kweli unafifia kimya na GIZA LA MACHAFUKO NA MATENGANO linaingia  huku wengine wakishangilia kana kwamba ndio kunapapmbazuka na tumaini jipya.

NINANI MWENYE JUKUMU?

UKISOMA KATIKA KITABU CHA YONA 1:1-4
Utaona YONA anatumwa kwenda kufanya kazi katika mji mmoja na YEYE KWA UKAIDI anaamua kwenda alipo taka yeye. Katika hali ile ya kulazimisha aende atakako akajikuta kawaingiza na wengine matatani bila kujijua.
Chombo alichopanda ili ajiepushe na USO (KUSUDI) WA BWANA MUNGU  KIKAPIGWA NA DHORUBA KALI kiwango ambacho kilizua hofu kwa waliomo katika chombo. Ikawa kila mtu akijaribu kumkumbuka na kumwomba MUNGU WAKE ili mambo ya tulie lakini aliye watumbukiza wengine kwenye kadhia hio alikua amelala
  

YONA 1:
4  Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.
5  Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi.
6  Basi nahodha akamwendea, akamwambia, UNA NINI, EWE ULALAYE USINGIZI? AMKA, UKAMWOMBE MUNGU WAKO; LABDA MUNGU HUYO ATATUKUMBUKA, TUSIPOTEE.


KWAHIO
Yona 1: 11  Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka.
12  Naye akawaambia, NIKAMATENI, MNITUPE BAHARINI; BASI BAHARI ITATULIA; KWA MAANA NAJUA YA KUWA NI KWA AJILI YANGU TUFANI HII IMEWAPATA.
13  Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana.


au
LUKA 21: 34  Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
35  kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
36  BASI, KESHENI NINYI KILA WAKATI, MKIOMBA, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.

Mimi na wewe tunaweza tukaamua kusimama katika nafasi zetu na kuamua  kumuomba mungu atusaidie kwa ajili ya nchi hii ili tusiingie katika machafuko na chuki kuu. Tuombe kwa moyo wa dhati kwaajili ya nchi yetu ili:-
-ISIINGIE KATIKA CHUKI ZA KIDINI NA KISIASA
-ISIINGIE KATIKA VITA NAN CHI JIRANI
-ISIINGIE KATIKA MIKATABA YA KINYONYAJI
-ISIINGIE KATIKA MIKATABA YA KISHOGA NA KISAGAJI NA YOTE YALIO CHUKIZO MACHONI PA MUNGU.

LAKINI KUMBUKA MAOMBI HAYA YOTE YANAANZA NA WEWE SIO LAZIMA YAANZE NA KIONGOZI WAKO WA KIDINI ILA UNAWEZA KUMSHAURI TU KAMA ATAONA NI VEMA ASHIRIKISHE NA JUMUIA KUBWA YA WATU

WARAKA WANGU KWA WAPENDWA WOTE

MARKO MANGARA MATHIAS

No comments:

Post a Comment