Saturday, August 10, 2013

KUTOKA KWA ZITTO KABWE

Sheikh Ponda Issa Ponda, nimejulishwa kwamba amefariki dunia kufuatia kushambuliwa kwa risasi na polisi huko Morogoro. Inna Lillah Wainna illaih raajiun.
Ninalaani kwa nguvu zote matumizi ya nguvu yanayofanywa na jeshi la Polisi dhidi ya Raia. Hili ni tukio lingine kati ya matukio yaliyotangulia kuhusu polisi kuua raia hovyo kwa kutumia risasi za moto. Ni lazima kuendelea kupambana na hali hii. Hata hivyo, ninaomba Watanzania wabakie watulivu kwani matukio kama haya ni majaribu makubwa kwa Umoja wa nchi yetu. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Sheikh Ponda Issa Ponda

No comments:

Post a Comment