Monday, July 1, 2013

UTAPELI


Ben Komba/Pwani-Tanzania/31/6/2013/09:45
Katika kile kinachoashiria kuwa heshima na utu wa mwanadamu unaporomoka kwa kasi, Mtanzania mmoja anayejulikana kwa jina la ABDUL RAMADHAN amefanya vitendo vya kitapeli kwa jamii ya waislamu wanaoishi katika maeneo ya Kibaha kwa Mathias mjini Kibaha.

Inasemekana kuwa siku ya Jumapili BW.ABDUL RAMADHAN alifika maeneo ulipo msikitini kwa lengo la kutaka usaidizi wa kumzika mtu ambaye alikuwa mfanyakazi wake wa nyumbani ambaye amefariki.

BW.RAMADHAN alimwambia Imamu SAID OMAR wa msikiti QADIRIYA kuwa yeye alikuwa anaishi na marehemu kama mfanyakazi wa nyumbani lakini kwa bahati mbaya mauti yamemkuta na hivyo angehitaji msaada wao ili kuweza kwenda kumsitiri marehemu.

Baada ya kumsikiliza kwa makini Tapeli huyo ambaye uso wake ulionyesha kila dalili za masikitiko na uchungu usio kifani alipatiwa msaada ambao aliutaka ikiwa pamoja na wachimba kaburi ambao walifanya kazi yao kwa ufasaha.

Ndipo wakati ukafika akamwambia Imam OMAR wa msikiti wa QADIRIYA kuwa itakuwa vyema kama wataenda Mochwari kwa ajili ya kuandaa mwili kwa ajili ya maziko kwa pamoja akiwemo na mpiga picha waliingia kwenye Taxi kuelekea mochwari.

Wakiwa njiani ABDUL RAMADHAN alimuomba simu ya mkononi Imam Yule aliyekuwa naye kwa madai ya kuwa simu yake imekata chaji, bila wasiwasi Imam akamkabidhi simu yake tapeli Yule, na bado wakiwa njiani tapeli Yule alimuomba mpiga picha kamera yake aangalie ambapo aliisifia kuwa ni nzuri na kutaka kuinunua.

Mara kabla hawajafika mochwari ya hospitali ya Tumbi, BW.ABDUL RAMADHAN alishauri ingekuwa vyema iwapo kwanza wangeenda kununua nyama kwa ajili ya chakula cha msibani, na kuelekea maeneo ya Mailimoja kwenye bucha ambapo aliagiza kilo 25, wakiwa pamoja na mpiga picha.

Baada ya kuzuga kwa muda kidogo tapeli Yule alimuaga mpiga picha kuwa anaenda kununua viungo vingine kama limao, nyanya na vitunguu kwa ajili ya mboga, ndipo alipokula kubwa mpaka muda huu.

Kutokana na hali hiyo mpaka ilipofika saa 12 jioni kulikuwa na kaburi wazi pasi marehemu wa kuzikwa akiwa hayupo, kutokana na utapeli wabinadamu wenye kupenda kutumikia njia ya mkato kufanikisha mambo.

No comments:

Post a Comment