Monday, July 22, 2013

BONANZA LA MICHEZO KINAMAMA KKKT.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/11:06

Wanawake wakristo nchini wamehimizwa kushiriki Bonanza la michezo kwa wanawake wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ambayo itakuwa inafanyika kila baada ya klipindi Fulani katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Bonanza hilo, BIBI. VERONICA KILEO amesema kuwa ni mara yao ya kwanza kuandaa bonanza hilo kwa lengo la kuhamasisha kinamama washiriki michezo.

BIBI.KILEO amefafanua kuwa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambayo ina kanda za kiusharika sita ndio zilizotakiwa kushiriki mashindano hayo lakini hata hivyo ni kanda nne tu zilizoshiriki Bonanza hilo, na kanda mbili za Zanzibar na magharibi zikishindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali.

BIBI.KILEO ameongeza kuwa michezo mbalimbali imeshindaniwa katika bonanza hilo ikiwa pamoja na mazoezi kupasha mwili moto (warmup) kwa takriban dakika 15,kukimbiza kuku, kuvuta kamba na mpira wa pete.

Mshauri wa kamati ya maandalizi ya Bonanza hilo Mama ANNA BAYI amesema hatua hiyo ambayo wameifikia ni nzuri katika suala zima la kuimarisha michezo upande wa kinamama.

Mama BAYI anaamini kuwa huo ni mwanzo tu, na anategemea mabonanza mengine yatakuwa bora zaidi kwani watatumia fursa hii kutambua mapungufu na kurekebisha upungufu huo ili kuweza kuhamasisha wanawake zaidi kujitokeza kushiriki.

No comments:

Post a Comment