Monday, July 22, 2013

KATIBU CCM KIBAHA MJINI ASHANGILIWA NA BAVICHA.Ben Komba/Pwani-Tanzania/22-07-2013/10:27
Katibu wa Chama cha Mapinduzi mwishoni mwa wiki amejikuta akipigiwa makofi na wananchama wa chama cha maendeleo na demokrasia wa mjini Kibaha baada ya kujitokeza na kusuluhisha mvutano uliopo wa kuzuia CHADEMA kufungua matawi katika maeneo mbalimbali mjini Kibaha.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia Katibu wa CCM Kibaha mjini, BIBI.MWAJUMA NYAMKA akitoka ofisini kwake akaenda moja kwa moja kwenye kundi la vijana wa CHADEMA ambao katika kipindi hicho walikuwa wanavutana na Diwani wa CCM kata ya Mailimoja, BW.ANDREW LUGANO ambaye alikuwa akizuia ujenzi huo.

Ambapo BIBI.NYAMKA kwa kutumia busara nadra sana kuonyeshwa na viongozi wa kisiasa, alimtaka diwani huyo kuwaacha waendele kufungua matawi kwani kinachoangaliwa na wananchi ni sera sio wingi wa matawi.

Naye Diwani wa Kata ya Maili moja kupitia tiketi ya CCM, BW.ANDREW LUGANO yeye kwa upande wake amezuia ujenzi holela wa matawi ya CHADEMA kwa sababu eneo ambalo wamefungua tawi limekuwa likitumika kwa ajili ya soko la jioni kwa wafanyabiashara ndogondogo.

Na afanyi hivyo kutokana na chuki au shinikizo ila kwa akili ya kawaida isiyo na mawaa dhidi ya chama au mtu yoyote binafsi, bali katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku kama diwani wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment