Friday, June 28, 2013

SUGU HURU

Leo (Juni 28, 2013) asubuhi, Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu) alipelekwa mahakamani kwa shitaka la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Waziri Mkuu, shtaka hili lilifunguliwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Dodoma na mwendesha mashitaka wa serikali.

Baada ya kufunguliwa shtaka hilo, Lissu ambaye alikuwa wakili wa Sugu aliitaka mahakama ifutilie mbali shtaka hilo kwani halina msingi wowote wa kisheria na baada ya mabishano ya kisheria baina ya Lissu na wanasheria wa serikali kushindwa kuthibitisha kuwa neno Mpumbavu ni lugha ya matusi, hakimu ameamua kufuta shtaka hilo na ametangaza kuwa Sugu yuko huru na hana kesi ya kujibu.

No comments:

Post a Comment