Sunday, April 28, 2013

MAPIGANO SUDANWakazi wa mji muhimu wa Sudan ambao ulishambuliwa na wapiganaji hapo jana, wamechoma moto majengo ya serikali na kuwarushia mawe wakuu wa jimbo.

Walikuwa wakipinga ziara ya gavana wa jimbo ambaye alizuru mji wa Umm Rawaba, kwenda kuona uharibifu uliosababishwa na mapigano.
Wapiganaji wa kundi la JEM na wapiganaji wengine waliuteka mji wa Umm Rawaba kabla haujakombolewa na jeshi la serikali.
Kawaida wapiganaji wa GEM wanaendesha harakati zao katika jimbo la Darfur.
Waandishi wa habari wanasema shambulio hilo lilikuwa la kijasiri kwa sababu limetokea katika jimbo la Kordofan Kaskazini, eneo ambalo lilikuwa halikuathirika na harakati za wapiganaji.
<

No comments:

Post a Comment