Monday, February 11, 2013

VIASHIRIA VYA UDINI GEITA

Taarifa za uhakika zilizonifikia kama saa moja hivi iliyopita zinaeleza kwamba mapigano yameibuka na yanaendelea kati ya Wakristo na Waislamu katika mji Mdogo wa Buselesele wilayani Chato Mkoani Geita wakigombania kuchinja.

Ni kwamba jana wakristo alitangaza kwenye mkutano wa hadhara kwamba leo jumatatu wanaanza kuchinja na kuuza nyama kwenye bucha zao,na wakaitangaza moja ya bucha zilizoko katikati ya soko la Mji wa Katoro kwamba ndilo litakuwa likiuza nyama za wakristo.

Ilipofika asubuhi ya leo majira ya saa 9 waislamu wakapata taarifa kwamba bucha hiyo inauza nyama kwa ajili ya wakristo,huku bucha zao zikionekana kudorora ambapo waliamua kwenda na kuanzisha vurugu kwenye bucha hiyo.

Kwa mujibu wa Taarifa hizo tayari aidi ya watu 10 wamejeruhiwa kwa kukatwa mapanga ambapo mmoja hali yake inaelzwa kuwa mbaya na amekimbizwa ktika hospitali ya wilaya ya geita,tayari polisi wa kikosi maalum cha kutuliza ghasia FFU kikiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Geita wamewasili eneo la tukio.

Nitaendelea kuwajuza kinachoendelea kadri nitakavyokuwa Napata tarifa ikiwa ni pamoja na picha za majeruhi.Kwa wale wenyeji wa eneo hilo ni vigumu kutofautisha mji wa Katoro wilayani Geita na Buselesele wilayani chato kwa sababu ni miji iliyoko kwenye eneo moja na inaingiliana kwa kila kitu.

No comments:

Post a Comment