Monday, February 11, 2013

CHADEMA YAENDELEA KUTESA KIBAHA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-Feb-13/13:42:54

Chama cha demokrasia na maendeleo kimewataka wananchi kutokubali kurubuniwa kwa kuwaambia CHADEMA ni chama cha kidini kunakosababishwa kwa baadhi ya vyama kutumia propaganda hiyo kutaka kuwagawa watanzania na baadaye kuwatawala kwa kufuata mifumo ya kurithishana kama inavyojidhihirisha hivi sasa.

Akiongea katika mkutano wa vuguvugu la mabadiliko inayoendelea nchi hivi sasakatika viwanja vya stendi ya Mzenga katika mamlaka ya mji mdogo wa Mlandizi yenye kulenga kutekeleza kauli ya mwaka wa nguvu ya umma inayoeendeshwa na chama cha demokrasia na kufanikiwa kuleta mitazamo chanya kwa wakazi wa wilaya ya Kibaha kutokana na kuwepo piga nikupige ya mikutano kati ya chama cha CHADEMA na CCM.

Kada wa chama cha demokrasia na maendeleo kutoka Arusha, BW.ALLY BANANGA amesema cha cha CCM kimekuwa chama cha kurithisha uongozi na kuyatupa kando malengo ya awali ya uanzishaji wa chama hicho ambayo yalikuwa hayana lengo la kujenga himaya za kisultani kwa baadhi ya viongozi na familia zao kama ilivyo hivi sasa kwa kuzusha mambo ambayo hayana ukweli wowote katika kujaribu kuwagawa watanzania kiimani.

BW. BANANGA amebainisha kumekuwepo na harakati kubwa katika kuhakikisha wanafanikiwa kukamata dola mwaka 2015 na kuwaasa wana Kibaha ambo wamechoka kunyanyaswa na kukandamizwa na chama tawala kuunga mkono harakati hizo za CHADEMA zenye lengo la kumkomboa mtanzania na mgogoro mkubwa wa kimfumo tunaokabiliana nao kutokana na baadhi ya watu kujiona kama wana hati miliki na Taifa hili.

No comments:

Post a Comment