Tuesday, February 5, 2013

MBINU MPYA ZA KUBEBA "MZIGO WA DAWA ZA KULEVYA" 

WAKATI NCHINI ZIMBABWE WANAWAKE WAKITUMIA PAMPERS KUKUZA UKUBWA WA MAKALIO YAO, NCHINI MAREKANI WAMEKUWA WAKITENGENEZA PAMPERS ZA COCAINE, AMBAZO HUVALIWA  NA KUSAFIRISHA DAWA HIZO NCHI MBALIMBALI PASIPO KUGUNDULIKA.

MBINU HIYO MPYA IMEDAIWA KUWAGHARIMU MUDA MREFU WAANDAAJI KUTENGENEZA PAMPERS HIZO NA BAADA YA KUKAMILIKA HUVALIWA KITAALAMU NJE YA NGUO ZAO ZA NDANI NA HUVALIA SURUALI AU BAIBUI TAYARI KWA KUANZA SAFARI.

MAOFISA WA FORODHA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA JFK WAMEGUNDUA MBINU HIYO MPYA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA BAADA YA KUWATIA MBARONI WANAWAKE WAWILI KUTOKA BRONX WAKIWA WAMEVALIA MADAWA HAYO. WANAWAKE HAO WAMEKAMATWA NA KILOGRAMU 6.5 ZA DAWA ZA KULEVYA AINA YA COCAINE AMBAZO WALIKUWA WAMEZIVALIA KWA MTINDO WA NEPI NJE YA NGUO ZAO ZA NDANI.

No comments:

Post a Comment