Tuesday, February 5, 2013

LILIPOFIKIA BUNGE LETU TZ
TAHARUKI IMEIBUKA LEO KATIKA UKUMBI WA BUNGE MJINI DODOMA LEO KUFUATIA MBUNGE JOHN MNYIKA WA JIMBO LA UBUNGE (CHADEMA)KUTOA HOJA YAKE BINAFSI BUNGENI NA BAADA YA MJADALA WAZIRI WA MAJI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE ALIHITIMISHA KWA KUOMBA HOJA HIYO IONDOLEWE BUNGENI KWANI HAIKUWA NA MASHIKO.

WAZIRI ALIFAFANUA KUWA SI KWELI KWAMBA SERIKALI HAIFANYI JITIHADA ZOZOTE ZA KUHAKIKISHA KUWA JIJI LA DAR ES SALAAM LINAKUWA NA MAJI SAFI NA SALAMA IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA VYEMA MIFUMO YA MAJI TAKA.

"NDUGU WABUNGE TUKISEMA KUWA HAKUNA KITU AMBACHO SERIKALI INAFANYA KUHUSU MAJI KAMA ALIVYOAINISHA MBUNGE MNYIKA, NI UONGO, UKWELI NI KWAMBA SERIKALI INAFANYA JITIHADA ZA MAKUSUDI ZA KUHAKIKISHA KUWA WANANCHI WAISHIO JIJINI DAR ES SALAAM WANAPATIWA HUDUMA BORA YA MAJI"ALISEMA PROFESA MAGHEMBE.

ALISEMA KWA KUWA SERIKALI IPO KWENYE UTEKELEZAJI WA MIKAKATI AMBAYO IMEELEZWA NA MNYIKA HAKUNA HAJA YA KUENDELEA KWA HOJA HIYO KWANI NI MUENDELEZO WA HOJA YA SERIKALI YA KUBORESHA SEKTA YA MAJI SAFI NA TAKA NCHI NZIMA.

AWALI MNYIKA ALITOA HOJA YAKE HIYO AKILITAKA BUNGE LIPITISHE HOJA HIYO ILI IWE MJADALA RASMI UTAKAO

SAIDIA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KUBORESHA SEKTA YA MAJI KWANI HIVI SASA KITU KINACHOFANYIKA NI UBABAISHAJI WA HALI YA JUU.

KUFUATIA HATUA HIYO BAADA YA YA SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI KUTAKA KURUHUSU HOJA HIYO KUONDOLEWA, WABUNGE WALIOKUWA WAKIMUUNGA MKONO MBUNGE MNYIKA WALIANZA KUPIGA KELELE JAMBO LILILOPELEKEA SPIKA WA BUNGE KUAHIRISHA BUNGE MAPEMA.

KABLA YA KUAHIRISHA BUNGE HILO WABUNGE HAO WALISIKIKA KWA NGUVU WAKISEMA CCM, CCM,CCM JAPO KUWA WALIOMBWA KUACHA NA KUTULIA KATIKA VITI VYAO HAIKUWEZEKANA, BAADA YA HALI HIYO SPIKA NDUGAI ALIMKARIBISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI HATA HIVYO HAIKUSAIDIA CHOCHOTE.

HALI ILIENDELEA KUWA TATA BUNGENI HAPO NDIPI SPIKA NDUGAI ALIPOTUMIA MWANYA BAADA YA KELELE KUPUNGUA KIDOGO KUWAULIZA WABUNGE KUWA WANAOKUBALI HOJA HIYO IONDOLEWE WASEMA NDIYO, WABUNGE UMATI MKUBWA WA CCM WAKAPIGA KELELE ZA NDIYO, NA ALIPOULIZA WANAOTAKA HOJA HIYO IENDELEE WABUNGE WAPINZANI WALISIKIKA KWA SAUMTI NDOGO WAKISEMA NDIYOOO,…HIVYO ALISEMA KUW AHOJA HIYO YA MNYIKA IMEONDOLEWA NA KISHA KULIAHIRISHA BUNGE.

No comments:

Post a Comment