Wednesday, February 6, 2013

LAW DAY.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/06-Feb-13/15:21:57

Wananchi na watendaji wametakiwa kuheshimu sheria bila kushurutishwa, ili kuweza kujenga utawala ambao utafuata misingi ya sheria bila upendeleo wala ubaguzi wowote ili kuweza kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya sheria katika mkoa wa Pwani, Hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mkoa wa Pwani, Mheshimiwa BAHATI NDESERUA amesema katika ujenzi wa utwala wa sheria ambao utazingatia haki ya kila mmoja bila kujali itikadi au uwezo wa mtu binafsi, kwani hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria kama Mwanafalsafa SOCRATES aliyewahi kusema "Mfalme hawezi kuwa chini ya mtu, bali ni chini ya Mungu na sheria".

Hakimu Mkazi mfawidhi mwandamizi, BI.NDESERUA ameongeza katika kuitafakari siku hii ni vyema kutambua utawala wa sheria ni bora kuliko uhuru binafsi, na maana halisi ya utawala wa sheria kila mmoja wetu anapaswa kutendewa haki bila kujali uwezo au itikadi, kwani mbele ya sheria sisi sote ni sawa.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi wa Polisi ULRICH MATEI amesema kuwa katika utawala wowote unaofuata misingi ya sheria kila mtu anakuwa na uhuru wa kuwa uhuru wa kufanya mambo ili mradi asivunje sheria zilizopo, ikiwa pamoja na kusihi mahali popote apatakapo isipokuwa kama kuna maagizo yoyote ya kisheria ikiwa pamoja na kukabiliwa na jinai.

No comments:

Post a Comment