"
Ninatoa Mwezi mmoja tu nataka Halmashauri ya Jiji la Arusha iwe safi
na hii kazi Mkurugenzi anapaswa kuifanya kwa haraka sana na sioni na
siko tiyari kupewa sababu yeyote ile ya kwa nini Arusha ni Chafu.
Na baada ya mwezi mmoja Mimi Mbunge nitaanza kukusanya takataka
mjini na kumpelekea Mkurugenzi ofisini kwake ili kama Hazioni wananchi
wamsaidie kuziona na ninaomba Wananchi wote nitakapotangaza tarehe
hiyo mjitokeze kwa wingi ili tuwasaidie Jiji kukusanya Takataka na
kumwaga mbele ya ofisi zao ili wajue kwa uhalisia kero ya uchafu Mjini .
Sasa kazi ni kwa vitendo na hakika najua Serikali ni lazima iwajibike kwa watu wa Arusha .
No comments:
Post a Comment