Monday, December 17, 2012

"ZE BLUUZ" YADUNDWA NA WAKORINTO WA BRAZIL Mchezaji wa Corinthians

KLABU YA CORRINTHIANS KUTOKA BRAZIL, IMESHINDA KOMBE LA KLABU BINGWA DUNIANI BAADA YA KUILAZA CHELSEA BAO MOJA KWA BILA KATIKA MECHI YA FAINALI ILIYOCHEZWA NCHINI JAPAN.
PAOLO GUERRERO ALIIFUNGIA CORINTHIANS, BAO HILO MUHIMU NA LA USHINDI.
HATA HIVYO CHELSEA, ILIPOTEZA BAFASI NYINGI ZA KUFUNGA WAKATI WA MECHI HIYO.
KATIKA MUDA WA ZIADA FERNANDO TORRES, ALIPOTEZA NAFASI NZURI SANA YA KUZAWAZISA LICHA YA KUWAPIKU WALINZI WA CORINTHIANS NA KUBAKIA KIPA PEKEE.
TORRES ALIJARIBU KUMCHENGA KIPA WA CORINTHIANS LAKINI KOMBORA LAKE LIKAWA HAFIFU NA KUDAKWA KWA URAHISI NA KIPA.
CHELSEA ILIMALIZA MECHI HIYO IKIWA NA WACHEZAJI KUMI BAADA YA GARY CAHIL, KUPEWA KADI NYEKUNDU BAADA YA KUMFANYIKA MADHAMBI MCHEZAJI WA CORRINTHIANS EMERSON.
BAO LA CHELSEA LILILOFUINGWA KWA KICHWA NA FERNANDO TORRES LILIKATALIWA NA HIVYO VIJANA HAO KUTOKA BRAZIL WAKAIBUKA NA USHINDI.

No comments:

Post a Comment