Wednesday, December 19, 2012

KATONGO AWABWAGA DEMBA, NA DROGBA TUZO YA BBC Chris  Katongo

NAODHA HUYO WA ZAMBIA MWENYE MIAKA 30 AMEMSHINDA DEMBA BA, DIDIER DROGBA, YOUNES BELHANDA NA YAHYA TOURE NA KUWA MSHINDI WA KWANZA KUTOKA KUSINI MWA AFRIKA KATIKA HISTORIA YA MASHINDANO HAYO.
ORODHA YA WASHINDANI HAO ILITENGAZWA NA WATAALAMU WA SOKA AFRIKA, AMBAO WAMEZINGATIA UMAHIRI WA MCHEZAJI, UWEZO WA KIUFUNDI NA USHIRIKIANO NA WACHEZAJI WENGINE.
NA IDADI KUBWA YA WATU WAMEPIGA KURA KUPITIA NJIA YA MTANDAO AU UJUMBE MFUPI HUKU ASILIMIA 40 KATI YAO WAKIMCHAGUA KATONGO, AMBAYE ANACHEZEA TIMU YA CHINA HENAN CONSTRUCTION.

No comments:

Post a Comment