Monday, December 17, 2012

KATIBA MPYA YA MISRI



 Wamisri wakipiga kura ya maoni Jumamosi

MATOKEO YASIYO RASMI YA KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA YA MISRI YANAONESHA HUENDA KATIBA IKAKUBALIWA NA WAPIGAJI KURA.
WAMISRI WAKIPIGA KURA YA MAONI JUMAMOSI

JUMAMOSI USIKU MAKAO MAKUU YA CHAMA KIMOJA KINACHOPINGA KATIBA HIYO, YALICHOMWA MOTO.

KWA MUJIBU WA CHAMA CHA MUSLIM BROTHERHOOD, CHA RAIS MURSI, KATIBA MPYA INAVOELEKEA ITAKUBALIWA NA ASILI-MIA-56 YA WAMISRI.

HIYO HESABU SIYO RASMI NA INATOKANA NA TAKWIMU ZA VITUO VYA KUPIGIA KURA AMBAVYO VIMEMALIZA KUHISABU KURA.

HATA HIVO, UPINZANI NAO UNAKUBALI MATOKEO HAYO.

NA SIKU ZA NYUMA BROTHERHOOD IMEKUWA HODARI KUTABIRI MATOKEO.

JUMAMOSI USIKU WAFUASI WA KATIBA MPYA WALISHAMBULIA OFISI ZA MOJA KATI YA VYAMA VIKUBWA VYA UPINZANI, CHAMA CHA WAFD, NA KUZICHOMA MOTO.

WATU WA UPINZANI WAMEWALAUMU WAFUASI WA KUNDI LA KIISLAMU LENYE MSIMAMO MKALI.

HIYO NI ISHARA NYENGINE KUWA HATA MATOKEO YA KURA YA MAONI YAKIWA WAZI KABISA, HAITOMALIZA MAANDAMANO NA MAPAMBANO NCHINI MISRI.

No comments:

Post a Comment