Tuesday, October 2, 2012

KATIKA BIBLIA

MITHALI 9:6  Enyi wajinga, acheni ujinga, mkaishi, Mkaende katika njia ya ufahamu.
7  Amkemeaye mwenye dharau hujipatia fedheha; Amkaripiaye mtu mbaya hujipatia aibu.
8  Usimkaripie mwenye dharau, asije akakuchukia; Mkaripie mwenye hekima, naye atakupenda.
9  Mwelimishe mwenye hekima, naye atazidi kuwa na hekima; Mfundishe mwenye haki, naye atazidi kuwa na elimu;
10  Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima; Na kumjua Mtakatifu ni ufahamu.

No comments:

Post a Comment