Monday, October 1, 2012

MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI VIJANA KUFANYIKA MJINI KIBAHA.

Ben Komba/Pwani--Tanzania/10/1/12/06:47:51 PM


TAASISI ISIYO YA KISERIKALI YA RIGHT TIME YENYE MASKANI YAKE KATIKA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA MLANDIZI, IMEANDAA MAONYESHO KWA BIDHAA NA HUDUMA KWA VIJANA WAJASIRIAMALI IKIWA NI MUENDELEZO MPANGO ULIODHAMINIWA NA SHIRIKA LA KAZI ULIMWENGUNI-ILO- WA KAZI NJE NJE.
...
AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI, MRATIBU WA MAONYESHO HAYO, BIBI. TUNSIIME KYANDO AMESEMA MAONYESHO HAYO AMBAYO YATAENDESHWA KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA BEST ALTERNATIVE CONSULTING AND MARKETING (BEACOM), YANATARAJIWA KUFANYIKA KATI YA TAREHE 4-6 OKTOBA KATIKA VIWANJA VYA MAILIMOJA MJINI KIBAHA.

BIBI. KYANDO AMEFAFANUA LENGO KUU LA MAONYESHGO HAYO NI KUKUZA, KUENDELEZA NA KUIMARISHA MTANDAO WA VIJANA WAJASIRIAMALI KATIKA KUWAWEZESHA KUBADILISHANA UZOEFU WA UZALISHAJI NA UTOAJI HUDUMA KWA MFUMO WA KISASA NA KUJIFUNZA MBINU MPYA ZA MASOKO KAMA NJIA KUU YA KUTENGENEZA AJIRA ZENYE TIJA NA STAHA KUPITIA UJASIRIAMALI NA KUJIAJIRI.

BIBI. KYANDO AMEONGEZA KUWA HAKUTAKUWEPO ADA YA USHIRIKI KWA KUZINGATIA WASHIRIKI WENGI AMBAO WANATEGEMEWA KUSHIRIKI MAONYESHO HAYO YA BIDHAA NA HUDUMA KUWA VIJANA, ILI KUTOA FURSA KWA WAO KUJIGHARAMIA USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI MAMBOI AMBAYO MSHIRIKI ATATAKIWA KUJIGHARAMIA MWENYEWE.

No comments:

Post a Comment