Tuesday, September 4, 2012

WAANDISHI WASHUTUMU POLISI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/09/2012


WAANDISHI MKOA WA PWANI WAMELAANI HATUA YA JESHI LA POLISI KUMUUA KWA MAKUSUDI MWANDISHI MWENZAO, MAREHEMU DAUD MWANGOSI WAKATI AKITEKELEZA MAJUKUMU YAKE YA KIKAZI.
...
KATIBU WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA PWANI, BW. JOHN GAGARIN AMESEMA KAMA INAVYOONEKANA KATIKA PICHA AMBAYO WAANDISHI WA HABARI WANAAMINI INAONGEA MANENO 1000, NDIVYO TUNAVYOFUNDISHWA DARASANI, INAYOONYESHA ASKARI AKIMLENGA BW. DAUD MWANGOSI WAZIWAZI.

BW. GAGARIN AMESHANGAZWA NA HATUA YA JESHI LA POLISI KUUNDA TUME YA KUCHUNGUZA MAUAJI HAYO, KWANI NI UPOTEVU WA FEDHA ZA UMMA BURE, KINACHOTAKIWA NI KUWAJIBIKA KWA VIONGOZI WA JESHI HILO, KWA KUANZIA NA YULE ALIYEMPIGA RISASI KWA MAKUSUDI.

WAKIZUNGUMZA KATIKA MAHOJIANO NA MWANDISHI WA HABARI HIZI, MMOJA WA WAANDISHI AMBAYE NIMEONGEA NAYE, BW. OMARY MNGINDO AMESEMA HATUA HIYO NI MBINU ZA MAKUSUDI ZA JESHI LA POLISI KUTAKA KUWATISHA WAANDISHI WASIFANYE KAZI YAO KWA WELEDI NA KUWAFANYA WANANCHI WASIHUDHURIE VIKAO VYA CHADEMA.

BW. MNGINDO AMESEMA LAZIMA IKUMBUKWE KUWA MWANDISHI ANA WIGO MPANA WA KUFANYA KAZI, NA KUCHUKULIWA MWANDISHI AKIONEKANA KATIKA MAANDAMANO YA CHADEMA AU WALIMU HAINA MAANA WAO NI WAHUSIKA WA KUANDAA MAANDAMANO YAO.

BALI WAO WAPO PALE KUTEKELEZA WAJIBU WAO, NA IKIONEKANA TAASISI YOYOTE INAKANDAMIZA KWA MAKUSUDI UTENDAJI WA KAZI WA WAANDISHI, BASI UJUE ANA UOZO AMBAO ANAFICHA KAMA INAVYOONEKANA KWA JESHI LA POLISI.

NAYE MRATIBU WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA PWANI, BI. MARGARET MALISA AMEITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA MADHUBUTI KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA MAUAJI YA RAIA WASIO NA HATIA.

No comments:

Post a Comment