Monday, September 24, 2012

UMOJA WA WAALIMU NCHINI KENYA WAFANIKIWA




KWA MARA YA KWANZA SERIKALI YA KENYA IMEKUBALI KUTOA NYONGEZA YA ASILI MIA 300 KWA MISHAHARA YA WALIMU AMBAO WAMEKUWA KATIKA MGOMO WA KITAIFA KWA WIKI TATU SASA.
KUTOKANA NA MAAFIKIANO HAYO KATI YA SERIKALI NA CHAMA CHA WALIMU NCHINI KNUT, SASA WALIMU WANATARAJIWA KUREJEA KAZINI JUMATATU.
HATUA HIYO SASA ITAWAPA AFUENI MAELFU YA WANAFUNZI HUSUSAN WA SHULE ZA MSINGI NA UPILI ZA UMMA AMBAO HAWAJAFUNZWA WAKATI HUU WALIMU WALIPOKUWA MGOMONI.
VYAMA VYA WALIMU NCHINI KENYA KNUT NA KUPPET VILIKUWA VIKISHINIKIZA SERIKALI KUWALIPA WALIMU NYONGEZA HIYO KWA AWAMU MOJA.

No comments:

Post a Comment