Monday, September 24, 2012

JOHN TERRY ASTAAFU SOKA
JOHN TERRY, NAHODHA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA SOKA YA ENGLAND, SIKU YA JUMAPILI ALITANGAZA KUSTAAFU KAMA MCHEZAJI WA KIMATAIFA.
TERRY, AMBAYE NI MLINZI WA KLABU YA CHELSEA, NA MWENYE UMRI WA MIAKA 31, ALITANGAZWA NA MAHAKAMA YA WESTMINSTER MJINI LONDON MWEZI JULAI KWAMBA HANA HATIA YA KUTUMIA MATAMSHI YA UBAGUZI WA RANGI DHIDI YA ANTON FERDINAND, TUKIO AMBALO LILIFANYIKA KATIKA MECHI YA LIGI KUU YA PREMIER.
LAKINI TERRY, AMBAYE ALISHIRIKI KATIKA MECHI 78 ZA KIMATAIFA, BADO HUENDA AKAADHIBIWA NA CHAMA CHA SOKA CHA FA, KUTOKANA NA UTOVU WA NIDHAMU, HUKU CHAMA KIKIENDELEA KUSIKILIZA KESI DHIDI YAKE SIKU YA JUMATATU.

No comments:

Post a Comment