Tuesday, September 25, 2012

MKWARA WA NIMRODI WA MSAIDIA

AMATI ya Usalama na Maadili ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imerudisha jina la Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kwenye Jumuiya ya Wazazi.
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya jina la mbunge huyo kutupwa na Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo na kusema hadharani kwamba akiachwa moja kwa moja, patachimbika. 
“Hapatatosha (CCM),” alisema Mkono alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusu kutoswa kwake katika mchujo wa awamu hiyo ya awali.

Katika matokeo ya mchujo huo wa awali uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam Mkono alishika nafasi ya mwisho kati ya wagombea 13, huku Abdallah Bulembo, Martha Mlata na John Barongo wakipitishwa.
Hata hivyo, Mkono ambaye ni wakili maarufu nchini, alipinga kushindwa katika kinyang’anyiro hicho akisema  bado mchakato wa uchaguzi unaendelea.

No comments:

Post a Comment