Tuesday, September 25, 2012

DK MGIMWA ATOA MISAADA


SIKU chache baada ya wanafunzi zaidi ya 100 kunusurika kufa baada ya mabweni matano ya Shule ya Sekondari ya St Mary kuteketea kwa moto, Mbunge wa Jimbo la Kalenga ambaye ni Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa amenunua vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh5.6 milioni ili kujenga mabweni hayo.
Vifaa hivyo ni bati 150, mifuko 100 ya simenti na makopo 30 ya rangi,  vitu ambavyo vitasaidia kukamilisha haraka ujenzi wa shule hiyo ambayo hivi sasa imefungwa kutokana na hasara kubwa waliyopata baada ya moto kuteketeza mabweni yake.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Lumuli, Wilayani Iringa, Dk Mgimwa alisema japo shule hiyo ni yabinafsi, kwa kuwa wanafunzi wanaosoma hapo ni watoto wa wananchi anaowaongoza lazima ahakikishe mabweni yanajengwa upya, ili wanafunzi warejee shuleni.

“Sijatoa vifaa hivi kisiasa, mkakati wetu mkubwa ni kutoa elimu bora kwa wananchi wetu bila kujali shule hii ni ya nani, nataka muda mfupi shule ifungue na kidato cha nne wanatakiwa kuwepo shuleni, ninachoomba kwenu wananchi ni ushirikiano ili tulinde mali zetu kuhakikisha hatuteketezi kiholela,”  alisema Dk Mgimwa.

No comments:

Post a Comment