Friday, September 7, 2012

MAJAMBAZI WAVAMIA BENKI NA KUIBAWATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAMEVAMIA NA KUTUMIA MBINU ZA UHALIFU WA HALI YA JUU NA KUPORA MAGUNIA YA FEDHA KUTOKA BENKI YA  BIASHARA YA AFRIKA (CBA), ILIYOPO  BARABARA YA NYERERE, JIJINI DAR ES SALAAM.

TUKIO HILO LINALOWEZA KUFANANISHWA NA FILAMU ZA KIMAFIA, LILITOKEA JANA KATI YA SAA 2.30 NA SAA 2.45 ASUBUHI. WALIONDOKA NA MAGUNIA HAYO WAKIWA WAMEYAPAKIA KWENYE MAGARI YAO YA KIFAHARI, BILA KUUA WALA KUJERUHI MTU.

KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM, SULEIMAN KOVA ALITHIBITISHA TUKIO HILO NA KUSEMA FEDHA WALIZOIBA ZINAKADIRIWA KUWA ZAIDI YA SH400 MILIONI.

“HATUFAHAMU KIASI KAMILI LAKINI, TULIVYOWAHOJI MAOFISA WA BENKI WANASEMA NI ZAIDI YA SH400 MILIONI AMBAZO ZIMEIBIWA,” ALISEMA KOVA.

ALIFAFANUA KWAMBA  TAYARI MENEJA WA BENKI, MSAIDIZI WAKE NA MLINZI ALIYEKUWA ZAMU WANASHIKILIWA NA POLISI KWA AJILI YA MAHOJIANO.

No comments:

Post a Comment