Thursday, September 6, 2012

KAMATI YA KUCHUNGUZA KIFO CHA MWANGOSI YAUNDWAWAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, DK EMMANUEL NCHIMBI AMEUNDA KAMATI YA WATU WATANO KUCHUNGUZA MAUAJI YA MWANDISHI WA HABARI WA KITUO CHA CHANNEL TEN, 


DAUDI MWANGOSI. (marehemu)


AKITANGAZA KAMATI HIYO DAR ES SALAAM JANA, DK NCHIMBI ALIWATAJA WAJUMBE WAKE KUWA NI JAJI MSTAAFU, STEVEN IHEMA AMBAYE ATAKUWA MWENYEKITI NA MWAKILISHI WA JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF), 

THEOPHIL MAKUNGA.

WAJUMBE WENGINE NI MWAKILISHI WA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT), 

PILI MTAMBALIKE, MTAALAMU WA MILIPUKO KUTOKA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ), KANALI WEMA WAPO NA NAIBU KAMISHNA WA POLISI (DCP), 

ISAYA MNGULU.

 MWANGOSI ALIFARIKI SEPTEMBA 2, MWAKA HUU BAADA YA KUPIGWA NA KITU KINACHOSADIKIWA KUWA NI BOMU WAKATI POLISI WALIPOKUWA WAKIWADHIBITI WAFUASI WA CHADEMA. “KAMATI HII NATAKA INIPE MAJIBU NDANI YA SIKU 30 NA KAMA UTAALAMU UTAKUWA HAUTOSHI TUTAOMBA MSAADA NJE,” ALISEMA DK NCHIMBI.

No comments:

Post a Comment