Wednesday, September 5, 2012

LIGI YA MABINGWA BARAN AFRIKA


ESPERANCE YA TUNISIA IMEMALIZA IKIWA KINARA WA KUNDI A LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA KUICHAPA SUNSHINE STARS YA NIGERIA BAO 1-0.
HUO NI USHINDI WA 19 KWA VIGOGO HAO WA TUNISIA WANAOSAKA KUTIMIZA NDOTO YAO YA KUTETEA UBINGWA WAO MSIMU HUU.

BAO PEKEE LA ESPERANCE LILIPATIKANA BAADA YA JUDE EBITOGWA KUJIFUNGA MWENYEWE WAKATI AKIJARIBU KUONDOA HATARI LANGONI MWAKE DAKIKA SABA BAADA YA KUANZA MCHEZO. SUNSHINE WAKIFUZU KAMA WASHINDI WA PILI.

ESPERANCE IMEFIKISHA POINTI TISA WAKIWA NA MECHI MOJA YA UGENINI DHIDI YA VIBONDE ASO CHLEF YA ALGERIA ITAKAYOCHEZWA KATIKATI YA MWEZI HUU, HUKU SUNSHINE IMEMALIZA IKIWA NA POINTI SITA.

ETOILE SAHEL YA TUNISIA IMEONDOLEWA MASHINDANO NA SHIRIKISHO LA SOKA AFRIKA CAF BAADA YA MASHABIKI WAKE MARA MBILI KUVAMIA UWANJA KWENYE MCHEZO DHIDI YA ESPERANCE.

ESPERANCE ITACHEZA NA MSHINDI WA PILI WA KUNDI B KATIKA NUSU FAINALI NA SUNSHINE WATACHEZA KINARA WA KUNDI HILO.
TP MAZEMBE YA DR CONGO NA AL AHLY YA MISRI ZIMEFUZU KWA HATUA YA NUSU FAINALI, LAKINI WANASUBIRI MECHI ZAO ZA MWISHO KUAMUA NANI ATAKUWA WA KWANZA AU WA PILI.

MAZEMBE WANAWEZA KUBAKI KILELENI MWA KUNDI KAMA WATAISHINDA BEREKUM CHELSEA YA GHANA NA MATOKEO TOFAUTI YA ACCRA YATAIPA NAFASI AHLY KUMALIZA KINARA KAMA WATAIFUNGA ZAMALEK.

No comments:

Post a Comment