Wednesday, August 22, 2012

MELES ZENAWI 1956 - 2012WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA, MELES ZENAWI (57), AMEFARIKI DUNIA JUZI USIKU MJINI BRUSSELS, UBELGIJI ALIKOKUWA AKITIBIWA.TAARIFA ILIYOTANGAZWA NA TELEVISHENI YA TAIFA YA ETHIOPIA, IMEELEZA KUWA ZENAWI ALIFARIKI DUNIA SAA 5:15 USIKU.

KUTOKANA NA KATIBA YA NCHI HIYO, NAFASI YA KIONGOZI HUYO MWENYE HISTORIA YA KIPEKEE NCHINI HUMO, ITASHIKILIWA NA NAIBU WAZIRI MKUU, HAILEMARIAM DESALEGN.

MPAKA ANAKUTWA NA MAUTI, HAKUNA TAARIFA ZOZOTE AMBAZO ZILITHIBITISHA HASA UGONJWA ULIOSABABISHA KIFO CHAKE. KIONGOZI HUYO ALIKUWA MADARAKANI TANGU MWAKA 1991 ALIPOMPINDUA MENGISTU HAILE MARIAM.
HATA HIVYO, TAARIFA AMBAZO HAZIJATHIBITISHWA ZINAELEZA KUWA ZENAWI ALIKUWA AKISUMBULIWA NA UVIMBE KWENYE UBONGO

No comments:

Post a Comment