Tuesday, August 21, 2012

MCHAKATO WA SENSA



Ben Komba/Pwani-Tanzania/8/21/
2012 1:21:10 AM

BAADHI YA WAISLAMU NCHINI WAMEENDELEA KUSISITIZA AZMA YAO YA
KUTOSHIRIKI SENSA KUTOKANA NA KUTOKUWEPO KIPENGERE CHA KUAINISHA DINI
KATIKA DODODSO HUSIKA KITU AMBACHO WAO WAMEAMUA KUTOKUBALIANA NACHO.

MWANANCHI ULEDI SELEMANI AMBAYE NI MUUMINI WA DINI YA KIISLAMU
ANAYESALI KATIKA MSIKITI WA MASJID NUUR ULIOPO KATIKA ENEO LA KIBAMBA
WILAYA YA KINONDONI, ANAELEZEA KUKWAZA KWAKE NA IMAM WA MSIKITI
KUWATAKA WAUMINI KUTOSHIRIKI SENSA.

BW. SELEMANI AMESEMA IMEKUWA DESTURI KILA BAADA YA SWALA YA “INSHA”,
MTOA MAWAIDHA KUSISITIZIA WAUMINI WA MSIKITI HUO KUSUSIA ZOEZI LA
SENSA IKIWA SEHEMU YA KUTEKELEZA MANUIZO YA WAISLAMU AMBAYO
WAMEAHIDIANA KUYAFANYA KUPINGANA NA SERIKALI KITU AMBACHO YEYE KAMA
MWISLAMU HAKUBALIANI NAYO.

AKISISITIZA MUUMINI MWINGINE BW. HAMZA KAGANGANA AMEBAINISHA YEYE KAMA
WAISLAMU WENGINE ANASEMA KITENDO CHA TBC KUTANGAZA WAKRISTO NI WENGI
KUPITA WAISLAMU KIMETETERESHA KWA KIASI KIKUBWA IMANI YAO NA UMATI WA
MTUME MUHAMMAD S.A.W.

AMEISHAURI SERIKALI IANGALIWE MATAKWA YA WAISLAMU ILI KUONDOA VUTA NI
NIKUVUTE ILIYOPO KATI YAO NA SERIKALI, NA KWA UPANDE WAKE SAUTI
ANAYOTAKA KUISIKIA AMBAYIO INAWEZA KUBADILISHA MSIMAMO WAKE LABDA
KUTOKA KWA TAASISI ZA KIISLAM NA JUMUIYA YA KIISLAMU YA ANSWAR SUNNA.

NAYE BI. MAYASA MZEE MKAZI WA MISUGUSUGU AMESEMA KWA UPANDE WAKE YEYE
ANAPENDA KUHESABIWA LAKINI KINACHOMTISHA NI HIVYO VITISHO WANAVYOPATA
KUTOKA VIONGOZI WAO WA MSIKITI NA WAKIWASHAURI KIFUNGU CHA QURAN
28:10-11 AMBACHO KINASSISITIZA KUPIGANIA IMANI YAO HATA IKIWEZEKANA
KUUA.

NAYE POLYCARP MAKUNGU AMESHANGAZWA HATUA YA WAISLAMU KUSUSIA SENSA
KUTOKANA NA MTU MMOJA TU KUTOA TAKWIMU AMBAZO SIO ZA KWELI, KITU
AMBACHO SIO MARA YA KWANZA KUFANYIKA NCHINI.

BW. MAKUNGU AMEELEZEA TUKIO LILILOFANYIKA SIO GENI, KWANI HATA AFISA
UHUSIANO WA BENKI YA STANBIC , BW. ABDALLAH SINGANO AMEWAHI KUNUKULIWA
NA VYOMBO VYA HABARI WAKATI WA UANZISHWAJI WA BENKI YA SHARIA AMBAPO
ALINUKULIWA AKISEMA UANZISHWAJI WAKE UMEZINGATIA UWEPO WA WAISLAMU
WENGI KUPITA WAKRISTO NCHINI, NA MBONA WAKRISTO HAWAKUANDAMANA.

HIVI KARIBUNI MKUU WA MKOA WA PWANI, BIBI. MWANTUMU MAHIZA AMEWAHIMIZA
WAISLAMU KUJITOKEZA KUSHIRIKI ZOEZI HILO NA KUJIEPUSHA NA WACHOCHEZI
AMBAO WANAJARIBU KUIFARAKANISHA SERIKALI NA WANANCHI WAKE KWA KIVULI
CHA UDINI JAMBO AMBALO SERIKALI HAITAKUBALI KULIONA LINAFANIKIWA.

BIBI. MAHIZA AMEFAFANUA KUWA MOJA YA NGUZO ZA KIISLAMU NI KUHESHIMU
MAMALAKA ILIYOPO MADARAKANI, NA HIVYO KUYATAKA MADHEHEBU YA KIISLAMU
KUFUATA TARATIBU ILI MADAI YAO YAWEZE KUSIKILIZWA NA SERIKALI.

NA AMEWATAKA VIONGOZI WA DINI KUACHA KUWATISHA WAUMINI WAO NA
WAJIANDAE KUHESABIWA HASA IKIZINGATIWA KUHESABIWA NI HAKI YAO YA
MSINGI BILA KUJALI IMANI AU KABILA YA MTU.

No comments:

Post a Comment