Wednesday, August 22, 2012

KAFUMU AFUMULIWA IGUNGA


CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) KIMEPATA PIGO BAADA YA MAHAKAMA KUU KANDA YA TABORA, KUTENGUA MATOKEO YA UBUNGE JIMBO LA IGUNGA YALIYOMPA USHINDI MGOMBEA WAKE, 


DK DALALY PETER KAFUMU.

DK KAFUMU ALIIBUKA MSHINDI KATIKA UCHAGUZI MDOGO ULIOFANYIKA OKTOBA 2, MWAKA JANA KUZIBA NAFASI YA


ROSTAM AZIZ

 ROSTAM AZIZ 
AMBAYE ALIJIUZULU KWA MADAI KWAMBA ANAACHANA NA SIASA CHAFU NDANI YA CCM.
AKITOA HUKUMU HIYO, JAJI MARY NSIMBO SHANGALI ALISEMA MAHAKAMA ILIPOKEA MALALAMIKO 15 AMBAYO YALIRIDHIWA NA PANDE ZOTE MBILI, LAKINI BAADAYE YAKAONGEZWA MADAI MENGINE MAWILI HIVYO KUFIKIA 17.

“MADAI YALIYOPOKEWA NA MAHAKAMA NI 17 NA KATI YAKE IMETHIBITISHA MADAI SABA,” ALISEMA JAJI SHANGALI KATIKA HUKUMU HIYO.

 “NDUGU MWANDISHI KARIBU SINGIDA, MIMI NARUDI KUENDELEA NA SHUGHULI ZANGU ZA MADINI.”
SABABU ZA KUTENGUA MATOKEO
AJI SHANGALI ALIENDELEA KUELEZA KUWA MBUNGE WA TABORA MJINI, ISMAIL ADEN RAGE ALITANGAZA KUWA MGOMBEA WA CHADEMA ALIKUWA AMEJITOA KATIKA UCHAGUZI HUO, JAMBO AMBALO MAHAKAMA IMERIDHISHWA NA USHAHIDI ULIOKUWA UKITOLEWA.

JAJI SHANGALI ALITAJA HOJA NYINGINE ILIYOTUMIKA KUFUTA MATOKEO HAYO KUWA NI KAULI YA IMAMU SWALEH MOHAMED WA MSIKITI WA IJUMAA IGUNGA, KUWATANGAZIA WAUMINI WA MSIKITI HUO KUWA WASIKICHAGUE CHADEMA, KWA KUWA BAADHI YA VIONGOZI WAKE WAMEMDHALILISHA MKUU WA WILAYA YA IGUNGA, FATUMA KIMARIO.ALISEMA HOJA NYINGINE NI KATIBU MKUU WA CCM, WILSON MUKAMA KUDAI KUWA CHADEMA KILILETA MAKOMANDOO KATIKA UCHAGUZI HUO NA KUPANGA KUUVURUGA.

HOJA NYINGINE AMBAYO JAJI SHANGALI ALIIKUBALI NI UGAWAJI WA MAHINDI YA KUWAWEZESHA WAKAZI WA IGUNGA KUKABILIANA NA NJAA WAKATI WA UCHAGUZI HUO KWAMBA ULITUMIWA VIBAYA NA BAADHI YA WANASIASA KUWASHAWISHI WANANCHI WAWAPIGIE KURA.

JAJI HUYO ALIHOJI IWAPO WAKAZI WA JIMBO LA IGUNGA WALIKUWA NA NJAA SANA WAKATI WA UCHAGUZI HUO KIASI CHA VIONGOZI WA SERIKALI KUONA KUWA ULIKUWA WAKATI MWAFAKA WA KUGAWA MAHINDI HAYO.

KUHUSU HOJA YA UPANDE WA UTETEZI KWAMBA MGOMBEA WA CHADEMA, KASHINDYE ALIPASWA KUPELEKA MALALAMIKO HAYO TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC), ALISEMA SIYO YA MSINGI YANAYOWEZA KUMZUIA MLALAMIKAJI KUPELEKA MALALAMIKO HAYO KATIKA MAHAKAMA KUU NA HAKUNA KIFUNGU CHOCHOTE KINACHOMZUIA MLALAMIKAJI KUFANYA HIVYO.

KUTOKANA NA HALI HIYO, JAJI SHANGALI ALISEMA KUANZIA SASA JIMBO LA IGUNGA LIPO WAZI NA KWAMBA: “MILANGO IKO WAZI KWA WALALAMIKIWA KUKATA RUFAA IKIWA HAWAJARIDHIKA NA UAMUZI.”

HALI YA USALAMA KATIKA MAHAKAMA HIYO ILIKUWA IMEIMARISHWA, HUKU WAFUASI WA CHADEMA WAKIWA WENGI ZAIDI NA WAKIONEKANA KUWA NA FURAHA HASA BAADA YA KUTOLEWA KWA HUKUMU HIYO.DK SLAA


DK SLAA, 
BAADA YA HUKUMU HIYO, KATIBU MKUU WA CHADEMA, DK WILLIBROD SLAA ALISEMA: “MAHAKAMA IMEDHIHIRISHA YALE AMBAYO TUMEKUWA TUKISEMA KILA WAKATI KWAMBA CCM INATUMIA MABAVU.”

ALISEMA ANASHUKURU MAHAKAMA KWA KUTOA HAKI NA KUKUBALIANA NA CHADEMA KUWA CCM ILIGAWA VYAKULA KWA WANANCHI ILI KUWASHAWISHI WAWAPIGIE KURA.


PIA ALISEMA KWAMBA IMEUDHIHIRISHIA UMMA KAULI KWAMBA CCM KINATUMIA VIBAYA RASILIMALI ZA NCHI KATIKA MAMBO YA SIASA AKITOA MFANO WA MAWAZIRI KUWALAZIMISHA WATU WAWACHAGUE WAGOMBEA WAO.NAPE 
KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI WA CCM, NAPE NNAUYE ALISEMA ALIKUWA HANA TAARIFA KUHUSU HUKUMU YA KESI HIYO.
HATA ALIPOPATA TAARIFA KUHUSU MATOKEO HAYO, ALISEMA ATAKUWA TAYARI KUYAZUNGUMZIA PINDI AKIYAPATA KUTOKA KATIKA MFUMO WA CHAMA CHAO.“SIWEZI KUZUNGUMZIA MATOKEO YA HUKUMU UNAYONIAMBIA WEWE. NITAKUWA TAYARI PINDI NITAKAPOYAPATA RASMI KUTOKA KULE IGUNGA (CCM),” ALISEMA NAPE.

No comments:

Post a Comment