Wednesday, August 22, 2012

MAENDELEO YA USAJILI BARAN ULAYA
KLABU YA QUEENS PARK RANGERS IMEINGIA MKATABA NA KLABU YA REAL MADRID AMBAO UTAMRUHUSU MCHEZAJI RICARDO CARVALHO KUJIUNGA NA QPR KWA MKOPO MSIMU HUU.
MCHEZAJI HUYO MWENYE UMRI WA MIAKA 34, NA MCHEZAJI KIUNGO WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA URENO, ANATARAJIWA KUJADILIANA NA KLABU HIYO KUHUSU MALIPO YAKE KATIKA MUDA WA SAA 48 ZIJAYO.

HAPO JANA QPR ILIMSAJILI

 MICHAEL DAWSON 

KUTOKA KWA KLABU YA TOTTENHAM KWA KITITA CHA PAUNI MILIONI SABA NUKTA TANO.

MSHAMBULIAJI MATATA WA MANCHESTER UNITED

 DANNY WELBECK

 AMESAINI MKATABA MPYA WA MIAKA MINNE, NA SASA ATASALIA KATIKA KLABU HIYO HADI MWAKA WA 2016.
MCHEZAJI HUYO MWENYE UMRI WA MIAKA 21, ALIFUNGA MABAO KUMI NA SABA KUTOKANA NA MECHI 64 ALIZOICHEZEA MANCHESTER UNITED NA VILE VILE ALISHIRIKISHWA KATIKA KIKOSI CHA ENGLAND KILICHOSHIRIKI KATIKA MICHUANO YA KUWANIA KOMBE LA MATAIFA BINGWA BARANI ULAYA


ILE DILI YA KUWABADILI GIANPAOLO PAZZIN NA ANTONIO CASSANO IMEKAMILIKA. NA ANTONIO CASSANO AMESHA SAINI DILI YA MIAKA MIWILI ILI KUCHEZEA TIMU YAKE MPYA YA INTER-MILAN. WACHEZAJI HAWA AMBAO WALIWAHI KUCHEZA TIMU MOJA YA SAMPDORIA.CHA AJABU NI KUWA CASSANO ATAUNGANA NA PAZZIN MAZOEZINI BAADA YA CASSANO KUFAULU VIPIMO VYA AFYA

No comments:

Post a Comment