Thursday, July 12, 2012

MCHAKAMCHAKA WA RVP


 
KOCHA ARSENE WENGER AMEWAAMBIA MAOFISA WA ARSENAL KUHARAKISHA KUMALIZIKA SUALA LA  ROBIN VAN PERSIE HATA KAMA UAMUZI NI KUMUUZA.
WENGER ANATARAJIA KUKUTANA ANA KWA ANA NA VAN PERSIE SIKU CHACHE ZIJAZO KWA LENGO LA KUMSHAWISHI KUBAKI EMIRATES.

LAKINI KAMA ATASHINDWA KUFIKIA NAYE MAKUBALIANO, BASI ANATAKA AUZWE HARAKA.


PENGINE ITAKUA FAIDA KWA ALEX FERGUSON AMBAYE YUKO MJINI LONDON NA HUENDA AKATUMIA FURSA HIYO KUMSHAWISHI MSHAMBULIAJI 'ALIYEIKATAA' ARSENAL, ROBIN VAN PERSIE KWENDA MANCHESTER UNITED.

KOCHA FERGIE ANGEPENDA KUONA VAN PERSIE AKICHEZA SAMBAMBA NA WAYNE ROONEY KWENYE UWANJA WA OLD TRAFFORD.
BOSI HUYO WA UNITED ANATARAJIA KUWA MMOJA WA WAGENI WAALIKWA KWENYE SHEREHE YA CHAKULA CHA JIONI ILIYOANDALIWA NA LABOUR PARTY SPORTS KWENYE UWANJA WA  EMIRATES.
HABARI ZA NDANI, ZINADAI KUWA FERGIE BADO ANA NDOTO YA KUMSHAWISHI VAN PERSIE KWENDA UNITED HASA BAADA YA MADACHI HUYO KUKATAA KUSAINI MKATABA MPYA ARSENAL.


UNITED ITASHINDANA NA HASIMU WAKE MKUBWA KWENYE JIJI LA MANCHESTER, KLABU YA MAN CITY AMBAYO KWA MUDA MREFU IMETAJWA KUMTAKA NYOTA HUYO.


<

No comments:

Post a Comment