Thursday, July 12, 2012

FAINALI YA KOMBE LA URAFIKI U/TAIFA LEO

 
 VS MABINGWA WA SOKA NCHINI, SIMBA NA MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI, AZAM FC ZOTE JIJINI DAR ES SALAAM, LEO ZINA FURSA YA KUONGEZA MATAJI KWENYE MAKABATI YAO PALE ZITAKAPOPAMBANA KATIKA MCHEZO WA FAINALI WA KOMBE LA URAFIKI, UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.
MSHINDI KATIKA MCHEZO HUO ULIOZUA MVUTANO KATI YA KLABU HIZO MBILI ZA LIGI KUU BARA NA CHAMA CHA SOKA ZANZIBAR (ZFA), ATAJINYAKULIA KITITA CHA SH10 MILIONI, HUKU MSHINDI WA PILI AKIONDOKA NA SH5 MILIONI.
MVUTANO HUO ULITOKANA NA KLABU KUTAKA MCHEZO WAO WA  FAINALI UHAMISHIWE UWANJA WA TAIFA, DAR ES SALAAM KWA MADAI YA KUTORIDHIKA NA MAZINGIRA MABOVU YA UWANJA WA AMAN AMBAO UMEKUWA UKITUMIKA KWA MICHUANO HIYO.
HII ITAKUWA MARA YA PILI KWA TIMU HIZO KUKUTANA KWENYE MICHUANO HIYO VISIWANI, BAADA YA KUPAMBANA KWENYE HATUA YA MAKUNDI NA KWENDA SARE YA BAO 1-1.
SIMBA ILIFANIKIWA KUSONGA MBELE HATUA YA FAINALI BAADA YA KUIFUNGA TIMU YA VIJANA YA ZANZIBAR (U23) BAO 1-0, HUKU AZAM NAYO IKIITAMBIA SUPERFALCON KWA MABAO 3-2.

No comments:

Post a Comment