Saturday, July 7, 2012

HELIKOPTA ILIYOKUWA IKIBEBA VIFAA VYA UCHAGUZI YASHAMBULIWA


WATU WENYE SILAHA WEMEISHAMBULIA HELIKOPTA ILIYOKUWA IKIBEBA VIFAA VYA UCHAGUZI VITAKAVYOTUMIKA KWA AJILI YA KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA JUMAMOSI NCHINI LIBYA, MAAFISA WA NCHI HIYO WAMESEMA.
HELIKOPTA HIYO ILILAZIMISHWA KUTUA NJE YA MJI WA MASHARIKI WA BENGHAZI. TAARIFA AMBAZO HAZIJATHITISHWA ZINASEMA MTU MMOJA AMEFARIKI.
UTAMBULISHO WA WASHAMBULIAJI BADO HAUJAJULIKANA, LAKINI ENEO LA MASHARIKI MWA LIBYA LIMEKOSA UTULIVU KUTOKANA NA MAKUNDI YANAYOTAFUTA UHURU WA KANDA HIYO.
UCHAGUZI WA WABUNGE NI ZA KWANZA NCHINI HUMO BAADA MAREHEMU MUAMMAR GADDAFI KUPINDULIWA MWAKA JANA.
HABARI HIZI ZINAKUJA WAKATI WATU WENYE SILAHA WAMEFUNGA VITUO VITATU VYA KUUZA NJE MAFUTA KUPINGA UCHAGUZI HUO.
WATU HAO WAMEKASIRISHWA KWAMBA ENEO LA MAGHARIBI YA NCHI LIMEPEWA VITI 200 ZAIDI KATIKA BUNGE JIPYA IKILINGALISHWA NA ENEO LA MASHARIKI LENYE UTAJIRI WA MAFUTA.
KULINGANA NA SHIRIKA LA HABARI LA REUTERS, NUSU YA VITUO VYA LIBYA VYA KUUZA NJE MAFUTA VIMEFUNGWA KUTOKANA NA HALI HIYO.
"HELIKOPTA ILIYOBEBA MASANDUKU YA KURA ILIRUKA JUU ENEO LA HAWARI KUSINI MWA BENGHAZI AMBAPO ALIPIGWA KWA KUWA KUTUMIA SILAHA NDOGO," AFP LIMENUKUU SHIRIKA LA HABARI KANALI ALI AL-SHEIKHI LIKISEMA.
ALISEMA MTU MMOJA ALIUAWA, LAKINI SHIRIKA LA HABARI LA REUTERS LINAMNUKUU RASMI AKISEMA KUWA MTU MMOJA ALIYEKUWA NDANI YA HELKOPTA ALIJERUHIWA WAKATI HELIKOPTA ALIPOPIGWA KOMBORA LA KUTUNGULIA NDEGE.

No comments:

Post a Comment