Friday, July 6, 2012

TAKUKURU WATUA KIBAHA


 

MKURUGENZI WA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA TANZANIA, BW. EDWARD HOSEAH AMEWATAKA WAHUSIKA WA MASUALA YA KODI KUANGALIA UPYA VIWANGO VIWANGO VYA KODI VINAVYOPANGWA ILI KUPUNGUZA USHAWISHI WA UTOAJI NA UPOKEAJI RUSHWA NCHINI.

BW. HOSEAH AMESEMA HAYO WAKATI WA UZINDUZI WA JENGO LA TAASISI HIYO MJINI KIBAHA, AMBAPO AMEBAINISHA KUWA UWEPO WA KODI NYINGI KWA WAFANYABIASHARA IMEKUWA KICHOCHEO KIKUBWA CHA RUSHWA HASA KUTOKANA NA KODI HIZO KUMUUMIZA MFANYABIASHARA NA KUAMUA KUTUMIA RUSHWA ILI KUJIPATIA NAFUU.

AKIZUNGUMZIA JUU YA JENGO HILO AMESIFU USHIRIKIANO ULIOONYESHWA NA TAASISI NYINGINE KUWEZESHA UJENZI WA JENGO HILO AMBALO LIMEGHARIMU TAKRIBANI SHILINGI BILIONI MOJA ZA KITANZANIA, NA AMEAAHIDI PCCB TAIFA KUTOA SAMANI NA FEDHA ZA KULIENDESHA JENGO HILO AMBALO NI MOJA KATI YA MAJENGO 8 YALIYOJENGWA NA PCCB, KATI YA HAYO MANNE NI OFISI ZA WILAYA.

AKIMWAKILISHA MKUU WA MKOA WA PWANI, KATIBU TAWALA WA MKOA, BI. BERTHA SWAI AMEWATAKA WATUMISHI WA TAASISI HIYO KUFANYA KAZI KWA KUFUATA MISINGI YA HAKI NA UADILIFU BILA KUMUONE AU KUMPENDELEA MTU YOYOTE ILI KUFIKIA MALENGO YA UWEPO WA TAASISI HIYO.

AIDHA AMEIPONGEZA TAASISI HIYO KWA KUFANIKIWA KUWAKAMATA BAADHI YA WATUHUMIWA WA MAKOSA YA RUSHWA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI, HATUA MABAYO INALETA MATUMAINI KWA JAMII.

No comments:

Post a Comment