Monday, July 9, 2012

CHADEMA,KIMETOA TUHUMA NZITO


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA),KIMETOA TUHUMA NZITO 
KIKIDAI KIGOGO MMOJA (JINA TUNALO) WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA ANARATIBU MPANGO WA KUWAUA VIONGOZI WAKE WAANDAMIZI AKIWAMO KATIBU MKUU, DK WILLBROD SLAA NA MBUNGE WA UBUNGO, JOHN MNYIKA.
MBOWE
KWA SABABU HIYO, CHAMA HICHO KIMEITISHA KIKAO CHA KAMATI KUU (CC) LEO KUJADILI MAMBO MBALIMBALI NA MWENYEKITI WAKE, FREEMAN MBOWE AMESEMA AJENDA KUU ITAKUWA KUZUNGUMZIA USALAMA WA VIONGOZI WAO KUTOKANA NA VITISHO HIVYO.

 MKUCHIKA

TUHUMA HIZO NI NZITO NA NITAZIJIBU KWA MAANDISHI.NJAMA HIZO ZIMEKUJA BAADA YA KUSEMEKANA KUNA SIRI AMBAZO ZINAENDELEA NDANI YA CHADEMA NA MWENYEKITI ANAJIBU

“SISI CHADEMA HATUNA MAMBO YA SIRI TUNAYOTAKA KUFANYA KATIKA NCHI HII. MATATIZO YA WATANZANIA YAPO WAZI NA YANAJULIKANA NA KILA MMOJA, SERIKALI YA CCM ITEKELEZE SERA NA AHADI ZAO KWA WANANCHI NA SI VITISHO, TUNAOMBA WANANCHI WAELEWE KUWA VIONGOZI WAO WAKO HATARINI, LAKINI CHADEMA HATUTARUDI NYUMA KATIKA KUTETEA HAKI  ZA WANYONGE HATA KWA KUFA NA HATUWEZI KUPELEKA MALALAMIKO YETU POLISI SABABU NAO NI SEHEMU YA TATIZO. ”

DR SLAA


CHADEMA KIMEAMUA KUTOTOA MADAI YAKE POLISI AKIDAI KUWA IMEPOKEA MADAI MENGI KUTOKA KWA VIONGOZI NA WANACHAMA YA KUTENDEWA VISIVYO LAKINI HAKUNA HATA MOJA LILILOWAHI KUFANYIWA KAZI. “TAARIFA ZA SASA WANAANZA NA MNYIKA NA KUFUATIA MIMI, NINACHOSEMA WAFANYE WATAKAVYO HATUTAACHA KUFANYA KAZI YETU, HATA NILIPOIBUA TUHUMA ZA EPA NILIWAAMBIA WATUHUMIWA WENGINE WA SAKATA HILO NI USALAMA WA TAIFA,” ALISEMA DK SLAA.

MNYIKA

ANAMUACHIA MUNGU KWA KUWA NDIYE ALIYETOA UHAI HATA KWA HAO WANAOFIKIRIA KUTEKELEZA KITENDO HICHO.  “NILIPOPATA TAARIFA HIZI NIMEKUTANA NA VIONGOZI WANGU WA CHAMA NA JANA USIKU (JUZI), NILIKUTANA NA FAMILIA YANGU, KWA PAMOJA WAMENIAMBIA NIENDELEE NA KAZI HII NINAYOIFANYA KWANI NIMETUMWA NA WANANCHI NA SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU, ”

“NILIPIGIWA SIMU NA MTU MMOJA KUTOKA SERIKALINI ALIYENIAMBIA KUNA GARI NYUMA LINANIFUATILIA, NILIPOGEUKA NILIONA NA KUSIMAMA KISHA NIKASHUKA NA KUBADILI GARI NA LENYEWE LIKAENDELEA KUNIFUATILIA KATIKA GARI NILILOKUWA NIMEPANDA,” ALIDAI  LEMA.

LEMA

LEMA ALIDAI KWAMBA HATA JUZI ASUBUHI ALIKUTANA NALO KATIKA NYUMBA ALIYOFIKIA NA ALIPOLIKARIBIA WATU HAO WALISHUSHA VIOO NA KUMSALIMU WAKIMWITA NI MBUNGE WA ARUSHA ALIYEKO KWENYE LIKIZO.

No comments:

Post a Comment