Monday, July 9, 2012

KABLA YA MGOMO WANAANZA KULUMBANA WENYEWE..........


CHAMA CHA WALIMU TANZANIA (CWT), KIMEWATAKA WALIMU KUUPUUZA UMOJA WA MAOFISA ELIMU TANZANIA (UMET) UNAOENEZA PROPAGANDA KWAMBA VIONGOZI WA CHAMA HICHO WAKO UPANDE WA SERIKALI HIVYO HAWAWEZI KUSIMAMIA KIKAMILIFU KUDAI MASLAHI YA WALIMU.
KAULI HIYO ILITOLEWA JANA JIJINI DAR ES SALAAM NA KATIBU MKUU WA CWT, EZEKIEL OLUOCH, KATIKA TAARIFA YAKE KWA VYOMBO VYA HABARI,.
“MOJA KATI YA TUHUMA ZINAZOTOLEWA NA UMET NI KWAMBA VIONGOZI WA CWT WANAPOKUTANA NA SERIKALI WANAMALIZANA, LAKINI HUKU NJE WANADAI HAWAJAELEWANA NA SERIKALI, HII SI KWELI HATUELEWI MAOFISA ELIMU WANA LENGO GANI,” ALISEMA.
ALISEMA CHAMA HICHO NI MAKINI KWANI KABLA YA KUTANGAZA MGOMO LAZIMA KIFUATE SHERIA ZINAZOTAWALA UTUMISHI WA UMMA KATIKA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA WALIMU.

No comments:

Post a Comment