Friday, July 6, 2012

CCM TANGA WASUSIA MWENGE

 

KATIKA HALI ISIYO YA KAWAIDA, CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) MKOANI HAPA KIMESUSA KUSHIRIKI KATIKA MAPOKEZI YA MBIO ZA MWENGE ULIOANZA KUKIMBIZWA MKOANI TANGA JUZI.
MWENGE HUO ULIOPOKEWA WILAYA YA PANGANI UKITOKEA MKOA WA PWANI, VIONGOZI WA CCM, NGAZI YA MKOA NA WILAYA HAWAKUONEKANA KATIKA SHUGHULI HIZO JAMBO LILILOZUSHA MASWALI MENGI KWA WANANCHI. CCM KABLA NA HATA BAADA YA KUINGIA KWA MFUMO WA VYAMA VINGI VYA SIASA, IMEKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA SHUGHULI ZOTE ZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, IKIZITUMIA JUMUIYA ZAKE NA HASA ILE YA UMOJA WA VIJANA KUSHIRIKI KIKAMILIFU TANGU MWANZO HADI MWISHO WA MBIO HIZO. MWENYEKITI WA CCM WA MKOA WA TANGA, MUSSA SHEKIMWERI, ALIPOULIZWA JUU YA HATUA HIYO, ALIKATAA KUZUNGUMZA AKIDAI KUWA KATIBU WAKE, GUSTAV MUBA, NDIYE ATAKAYETOA TAARIFA HIZO. HATA HIVYO, MUBA ALIPOULIZWA NA KUAMBIWA KUWA MWENYEKITI WAKE NDIYE ALIYEMTAKA ATOE KAULI, ALISEMA KUWA CHAMA HAKINA MAELEZO, BADALA YAKE AKADAI KUWA MSEMAJI WA JAMBO HILO NI MKUU WA MKOA, CHIKU GALLAWA.

No comments:

Post a Comment