Thursday, July 5, 2012

GOAL-LINE TECHNOLOGY


SHIRIKISHO LA MCHEZO WA SOKA DUNIANI FIFA LINAJIANDAA KUPIGA KURA KUIDHINISHA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA-MAARUFU KAMA GOAL LINE TECHNOLOGY- ITAKAYO TUMIKA KUAMUA IKIWA MPIRA UMEVUKA MSTARI WA GOLI AU LA.
KUMEKUWA NA SHINIKIZO CHUNGU NZIMA KWA SHIRIKISHO LA FIFA KUFUATIA MAKOSA KADHAA YANAYOHUSIANA NA MAAMUZI YA MECHI, IKIWEMO KOSA LA HIVI KARIBUNI KUHUSU MECHI MOJA WAKATI WA MICHUANO YA KUWANIA KOMBE LA MATAIFA BINGWA BARANI ULAYA.
GOLI LILILOFUNGWA NA UKRAINE DHIDI YA UINGEREZA ILIFUTILIWA MBALI LICHA YA PICHA ZA RUNINGA KUONYESHA KUWA MPIRA ULIKUWA UMEVUKA NA KUPITA MSTARI WA GOLI.
SHIRIKISHO LA FIFA LINATARAJIWA KUIDHINISHA MIFUMO MIWILI, MOJA INAYOTUMIA KAMERA ZA VIDEO NA NYINGINE INAYOTUMIA SENSA MAALUM ILI KUBAINISHA IKIWA MPIRA UMEVUKA MSTARI WA GOLI.

No comments:

Post a Comment