Thursday, June 21, 2012

WASOMALI WAMALIZA KIKAO


WAAKILISHI KUTOKA NCHINI SOMALIA NA SOMALILAND ILIYOJITENGA NA SOMALIA ZAIDI YA MIAKA ISHIRINI ILIYOPITA, WAMEKAMILISHA MAZUNGUMZO YAO YA KWANZA YA ANA KWA ANA NA YALIYOANDALIWA NA SERIKALI YA UINGEREZA.
MWANDISHI WA BBC ANASEMA KUWA MAZUNGUMZO HAYO YALINUIA TU KUTAYARISHA PANDE HIZI MBILI KWA MIKUTANO YA BAADAYE LAKINI YANGALI YATAONEKANA KAMA HATUA MUHIMU KATI YA NCHI HIZO MBILI.
SOMALIA NA SOMALILAND ZIMEKUBALI KUSHIRIKIANA KATIKA KUKABILIANA NA TATIZO LA UHARAMIA SWALA LA SIASA KALI PAMOJA NA MAMBO MENGINE MUHIMU.
PIA WAMEKUBALIANA KWAMBA MAZUNGUMZO YAENDELEE NA KISHA KUTOA WITO KWA MARAIS WA NCHI HIZO MBILI KUKUTANA .

No comments:

Post a Comment