Friday, June 29, 2012

VURUGU NAMANGA JIJINI DAR-ES-SALAAM


 

PALE NAMANGA KUNA SHELI YA BIGBON IKO BARABARANI KWA NYUMA YAKE AMEPAKANA NA NYUMBA ZA WANAKIJIJI, SASA YEYE ANADAI KANUNUA HILO ENEO LOTE NA ANAMILIKI HATI WANAKIJIJI WAMESEMA HAWAMTAMBUI WALA HAWAJAWAHI KUUZA KWA MTU ENEO HILO, KESI ILIKWENDA BARAZA LA ARDHI KWA MBINU NA HILA AKAFANIKIWA KUSHINDA KWANI BARAZA HILO HALINA HAKI KISHERIA YA KUSIKILIZA KESI HIYO.

WANANCHI WAMEAMUA KUIPELEKA KESI MAHAKAMA KUU NA WAMESHATOA NOTISI YA SIKU 90 KWA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ILI KUISHITAKI WIZARA YA ARDHI, KUNA KESI NYINGINE YA MADAI AMESHTAKIWA MAHAKAMA KUU KITENGO CHA ARDHI NA MZEE MMOJA AMEPAKANA NAE KWENYE HILO ENEO KWA KUMUINGILIA NA KUHARIBU MALI ZAKE ZOTE KWA KUDAI (BIGBON) KUWA ENEO HILO NI LAKE. KESI IMEPANGWA KUSIKILIZWA JULY.

LEO HII BIGBON AKIJUA FIKA KUA KUNA KESI MAHAKAMANI NA HAZIJASIKILIZWA BADO AMEPELEKA KIKUNDI CHA MABAUNSA KWENDA KUVAMIA KWA NGUVU ENEO HILO LA WANAKIJIJI KWA LENGO LA KUWATOA, NDIPO VITA KALI BAINA YA MABAUNSA HAO NA WANAKIJIJI ILIPOZUKA KWA TAARIFA NILIZOZIPATA, ZAIDI YA MABAUNSA WANNE WAMEULIWA NA WANAKIJIJI ILA KWASASA HALI IMETULIA.
WAKATI VURUGU HIZO ZIKIENDELEA NA MSAFARA WA RAIS ULIKUWA UKIPITA MAENEO HAYO HAKUNA UHUSIANO WOWOTE KATI YA VURUGU HIZO NA MSAFARA HUO, ILA ILIKUA NI JAMBO LA HERI KWANI MSAFARA HUO ULISAIDIA KUZIMA VURUGU HIZO BAADA YA ASKARI WA FFU KUFIKA KATIKA ENEO HILO NA KUANZA KUTAWANYA WATU...
SOURCE: TAARIFA KUTOKA KWA MZEE MMOJA MWANAKIJIJI AMBAE NAE NI MMOJAWAPO KATI YA WANAKIJIJI WANAOGOMBANIA ENEO NA BIGBON

No comments:

Post a Comment