Friday, June 29, 2012

RAIS WA ZANZIBAR ALONGA KUHUSU MUUNGANO


 

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT ALI MOHAMED SHEIN AMESEMA ATAENDELEA KUUTETEA MUUNGANO NA HAKUNA ATAKAEMLAGHAI WALA KUMCHEZEA KATIKA UONGOZI WAKE. KAULI HIYO AMEITOWA JANA KATIKA MKUTANO WA JUMUIYA YA WASTAAFU WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ULIOFANYIKA BWAWANI MJINI UNGUJA. DK SHEIN AMESEMA KWAMBA YEYE NDIE RAIS WA ZANZIBAR NA NDIE MWENYE MAMLAKA NA HATOMUOGOPA MTU WALA KUSITAKUWACHUKULIA HATUA KWA WALE WOTE AMBAO WATAKWENDA KINYUME NA MATAKWA YA KIKATIBA. ALISEMA KUWA DHAMANA YANCHI HII PAMOJA NA ILE YA JAMHURI YA MUUNGANO IMO MIKONONI MWAO KATI YAKE NA RAIS JAKAYA KIKWETE NA NDIO MAANA WAKAWA WANASHIRIKIANA NA KUSHAURIANA KWA YALE YOTE AMBAYO YANA MASLAHI NA NCHI. “KATIKA KUIONGOZA ZANZIBAR MIMI NDIE RAIS SIMUOGOPI MTU YEYOTE”, ALISEMA KWA KUJIAMINI DK SHEIN.

No comments:

Post a Comment