Wednesday, June 27, 2012

SIKUFANYA MAKOSA KUTUA JANGWANI.KELVIN YONDANI ALIYEJIUNGA YANGA TOKA SIMBA, AMESEMA KATIKA KIPINDI KIFUPI ALICHOFANYA MAZOEZI KLABU YAKE HIYO MPYA, AMEBAINI KUWA HAKUFANYA MAKOSA KUTUA JANGWANI.
YONDANI ALISEMA KUWA, MAISHA YA JANGWANI NI MAZURI HASA UKIZINGATIA KUWA AMEPATA MAPOKEZI NA USHIRIKIANO MZURI NA WACHEZAJI NA VIONGOZI.
PIA AMETUMIA FURSA HIYO KUITAKA SIMBA KUMSAHAU KWANI YEYE TAYARI NI MALI YA YANGA NA HAKUNA JITIHADA ZOZOTE ZA KUJARIBU KUMRUDHISHA SIMBA ZITAKAZOFANIKIWA.
UHAMISHO WA YONDANI ULIZUA UTATA MKUBWA BAADA YA KLABU YAKE YA ZAMANI KUDAI NI MCHEZAJI WAO HALALI, HUKU YANGA NA MCHEZAJI WENYEWE WAKISEMA TOFAUTI.
"SIFAHAMU KWANINI SIMBA BADO WANAZUNGUMZA MAMBO HAYA. MIMI NIMESHAMALIZA KILA KITU NA YANGA, NI VIZURI WAKANIACHA NIFANYE KAZI YANGA," ALISEMA YONDANI.

No comments:

Post a Comment