Wednesday, June 27, 2012

WAETHIOPIA 42 WAFA TANZANIA




WAHAMIAJI HARAMU AROBAINI NA WAWILI WAMEPATIKANA WAKIWA WAMEKUFA NDANI YA LORI WALIMOKUWA WAKISAFIRIA KATIKA MKOA WA DODOMA, NCHINI TANZANIA.
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA TANZANIA, PEREIRA SILIMA, AMESEMA KUWA WATU HAO WALIOKUWA WAMESONGAMANA NDANI YA LORI WALIAGA DUNIA KUTOKANA UKOSEFU WA HEWA SAFI.
''TAARIFA TULIYOPATA NI KWAMBA KULIKUWA NA WASAFIRI WALIOKUWA WAKISAFIRISHWA KWENYE LORI, AMBALO LILIKUWA KAMA KONTENA NA HALIKUWA NA HEWA YA KUTOSHA''.BWANA SILIMA
WAHAMIAJI WALIKUWA WANATOKA ETHIOPIA

AMESEMA WAHAMIAJI HAO HARAMU KUTOKA ETHIOPIA WALIKUWA WAKIJARIBU KUINGIA MALAWI.
KULINGANA NA BWANA SILIMA WAHAMIAJI HAO WALIANZA KUFARIKI DUNIA WAKIWA SAFARINI. JIHUDI ZA WAHAMIAJI HAO KUMJULISHA DEREVA KUHUSIANA NA HALI YAO HAZIKUFANIKIWA, NA HIVYO KUSABABISHA MAAFA YA WATU AROBAINI NA MOJA NDANI YA LORI HILO.
KULINGANA NA NAIBU WAZIRI HUYO WA MAMBO YA NDANI TUKIO HILO LILIFANYIKA JUMATATU USIKU. NA BAADA YA DEREVA HUYO KUGUNDUA KUWA WATU WAMEFARIKI, ALIONDOA MIILI YAO NA KUITUPA NJE KABLA YA KUTOWEKA.
MTU MMOJA ALIFARIKI DUNIA AKIFANYIWA MATIBABU KATIKA HOSPITALI YA MKOA MJINI DODOMA.
UHAMIAJI HARAMU UMEENEA

POLISI NCHINI TANZANIA WAMESEMA WANAMSAKA DEREVA HUYO AMBAYE ALITOROKA PUNDE TU BAADA YA KUSHUSHA MIILI YA WAHAMIAJI HAO HARAMU.
BIASHARA YA KUWASAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU HASA WANAOTOKA NCHI ZA SOMALIA NA ETHIOPIA KUPITIA TANZANIA IMEENEA SANA. WENGI HUELEKEA MATAIFA YA KUSINI MWA AFRICA KUTAFUTA MAISHA BORA.

No comments:

Post a Comment