Sunday, June 24, 2012

OLE SENDEKA HAMTAKI AMPINGA MWEKEZAJI

MBUNGE WA JIMBO LA SIMANJIRO, CHRISTOPHER OLE SENDEKA, AMEITAKA SERIKALI KUIFUKUZA NCHINI KAMPUNI YA TANZANITE ONE AMBAYO INACHIMBA MADINI YA TANZANITE MERERANI, ILI KUTEKELEZA SHERIA MPYA YA MADINI YA MWAKA 2010 AMBAYO INAELEZA WAZI KUWA MADINI YA VITO YANAPASWA KUCHIMBWA NA WAZAWA.
 
AKICHANGIA HOTUBA YA BAJETI  BUNGENI JANA NA BAADAYE KUTOA UFAFANUZI KWA MWANDISHI WA HABARI HIZI NJE YA BUNGE, SENDEKA ALISEMA KWA KUWA LESENI YA KAMPUNI HIYO, INAMALIZIKA JULAI MWAKA HUU, HIVYO HATEGEMEI LESENI HIYO KUTOLEWA TENA.
 
AKICHANGIA BUNGENI, SENDEKA ALISEMA SHERIA YA MADINI YA MWAKA 2010, INAELEZA KUWA MADINI YA VITO YANAPASWA KUCHIMBWA NA WAZAWA NA HIVYO SERIKALI INAPASWA KUTEKELEZA SHERIA HIYO.
 
SENDEKA ALIFAFANUA KUWA, SHERIA HIYO INAELEZA WAZI KUWA KAMA WAZAWA WANATAKA KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI KATIKA UCHIMBAJI WA MADINI HAYO, WAZIRI MWENYE DHAMANA BAADA YA KUFUATA TARATIBU KADHAA ZA KISHERIA NDIYE ANAYEWEZA KUTOA LESSENI.
 
HATA HIVYO NJE YA BUNGE, SENDEKA ALISEMA IMEKUWA NI KILIO CHA MUDA MREFU CHA WACHIMBAJI WADOGO KUKOSA MAENEO YA KUCHIMBA HIVYO, KAMA ENEO HILO LIKIREJESHWA KWA SERIKALI ITAKUWA NI FARAJA KUBWA.
 
ALISEMA KWA MAZINGIRA YA SASA, SIDHANI KAMA WIZARA ITAWEZA KUTOA LESENI MPYA YA UCHIMBAJI KWA KAMPUNI HIYO, AMBAYO IMEKUWA NA MIGOGORO WA WACHIMBAJI WADOGO KWA MUDA MREFU.
 
HATA HIVYO, HABARI ZA UHAKIKA TOKA NDANI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, ZILIELEZA JANA KUWA, HADI SASA BADO KAMPUNI HIYO HAIJAPEWA LESENI MPYA LICHA YA KUOMBA.
 
KAMPUNI HIYO YA TANZANITE ONE INAMILIKI ENEO LA KITALU C KATIKA MACHIMBO YA TANZANITE, HUKU WACHIMBAJI WADOGO WAKIWA WANAMILIKI ENEO LA KITALU A, KITALU B NA KITALU D AMBAYO HATA HIVYO MAENEO HAYO YENYE MSONGAMANO WA WACHIMBAJI WADOGO HAYANA UZALISHAJI KAMA ILIVYO ENEO LA KITALU C

No comments:

Post a Comment